Aliyekuwa
katibu mkuu Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesema
katika majukumu ya mwanadamu ni lazima kuwe na muda wa kufanyakazi na
kupumzika na hakuna jambo lisilo kuwa na mwisho.
Kinana
amesema hayo leo Mei 28, 2018 katika kikao cha wa halmashauri kuu Taifa
CCM (NEC) katika ukumbi wa mikutano Ikulu Jijini Dar es salaam wakati
wa kutangaza kustaafu nafasi ya Ukatibu Mkuu wa chama hicho na kuongeza
kuwa anashukuru wanachama na viongozi wa chama hicho kwa ushirikiano kwa
kipindi cha uongozi wake.
“Lazima
tukubali kuna wakati wa kufanyakazi na wakupumzika, naelewa ugumu
mnaoupata wa kutokunikubalia, tumekuwa na makatibu wakuu saba kwahiyo
sio ajabu katibu mkuu wa sasa kuanchia ngazi ili apatikane mwingine,
nashukuru mwenyekiti, makamu mwenyekiti na mzee Mangula kwa kunikubalia
na kutambua kuwa kila lenye mwanzo lazima liwe na mwisho”, amesema
Kinana.
Kinana
ameongeza kuwa amepokea simu na ujumbe mwingi katika simu yake za
wanachama na viongozi wa chama hicho wakimtaka kuendelea na nafasi ya
ukatibu mkuu.
0 comments:
Chapisha Maoni