Bunduki
ya kivita aina ya AK 47, ikiwa na risasi nne ndani imeokotwa ndani ya
vichaka katika Kijiji cha Naan, Wilaya ya Ngorongoro mjini Arusha.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Mei 29, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,
Ramadhani Ng’anzi amethibitisha kuokotwa kwa silaha hiyo na kuongeza
kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka mmiliki wake.
“Mbali
na bunduki hiyo, pia tumekamata pikipiki saba zinazodhaniwa kuwa ni
mali ya wizi na watuhumiwa saba kupitia msako tuliofanya hivi karibuni,”
amesema.
Kamanda
Ng’anzi amezitaja mali zilizokamatwa kuwa ni televisheni sita, camera
tatu, lensi mbili za camera, fedha taslimu Sh 915,000 na vitu vingine
vya ndani na vifaa ofisini.
Pamoja
na mambo mengine, Kamanda Ng’anzi amewaomba wakazi wa Arusha waliowahi
kuibiwa kufika kituoni hapo ili kukagua kama wanaweza kutambua mali zao.
0 comments:
Chapisha Maoni