Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amepiga
marufuku makampuni yanayopima ardhi yasiwadai wananchi gharama za
upimaji wa ardhi.
Amesema
kila makampuni hayo yatakapokuwa yakipima ardhi yatatakiwa kulipwa
fedha za upimaji kupitia kwenye vikundi vilivyochaguliwa na wananchi.
Lukuvi ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma leo, alipokuwa akiwasilisha bajeti ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2018/19.
“Aidha,
wapimaji hao wanatakiwa kutoa taarifa katika uongozi wa wilaya husika
kuhusu uwepo wao katika maeneo wanayopima ardhi,” amesema.
Pamoja
na mambo mengine, Waziri Lukuvi aliwahimiza wananchi kuwa na kawaida ya
kulipa kodi ya ardhi kila mwaka kwa kuwa ni wajibu wao kisheria.
“Kwa
upande wa wananchi wanaokabiliwa na migogoro ya ardhi, nawaomba wafike
kwa maofisa wa wizara yangu ili migogoro yao iweze kutatuliwa haraka
iwezekanavyo,” amesema Lukuvi.
0 comments:
Chapisha Maoni