Msanii
wa bongo fleva maarufu nchini , Diamond Platinumz kwa mara ya kwanza
amefunguka na kuzungumzia swala lake la kuachana na Zari na kumuomba
radhi mwanamama huyo ambapo taarifa za hapo awali ziliwahi kusema kuwa
kwa sasa Diamond amekuwa akipiga safari nyingi za Afrika ya Kusini ili
kuomba radhi kwa mwanamke huyo.
Akizungumzia
kuhusu vijembe vingi ambavyo diamond amekuwa akitupiwa na mwanamama
huyo hasa vya hapa karibuni alipokuwa kenya, Diamond alisema ; "hayo ya
kenya bwana tuachane nayo, mimi nadhani yameshapita naomba tuendelee na
haya yasasa itapendeza sana”
Hata
hivyo, mwandishi hakuishia hapo ndipo alipoamua kumuuliza moja kwa moja
kuhusu yeye kusafiri kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya kuomba radhi
kwa zari huku akienda kwa siri mara kwa mara na diamond alijjibu kuwa
safari zake za afrika ya kusini hazihusiani na mambo hayo.
"N
kweli ninaenda na so mara moja au mara mbili nimekuwa ninaenda,nakwenda
kule sio kwa ajili ya kumuomba msamaha , hapana ila ninakwenda kule kwa
ajili ya kuona wanangu tu,haiwezekani niwe ninatuma pesa za matumizi tu
alafu ninafka mpaka afrika ya kusini na nisiende kuwaona wanangu.
"Hao
wanaosema kuwa sijui nimekuwa nikimuangukia nadhani yatakuwa ni maoni
yao tu wala sio yangu, ni maneno yasiyokuwa na msingi, zari ni mama wa
watoto wangu na itabaki kuwa hivyo."
0 comments:
Chapisha Maoni