Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma
Serikali
imesema itaendeleza mapambano ya Vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi kwa
kuongeza kasi katika kuzuia maambukizi mapya ikiwemo kutoa elimu kwa
umma.
Akizungumza
jana mjini Dodoma wakati wa warsha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge inayoshugulikia Ukimwi na Madawa yakulevya Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu mhe. Jenista Mhagama
alisema kuwa dhamira ya Serikali baada ya kuanzisha mfuko wa Udhamini wa
Kudhibiti Ukimwi (ATF) ni kuhakikisha kuwa mfuko huo unajengewa uwezo
ili lengo la kuanzishwa kwake litimie.
“Tayari
mfuko umeweza kukusanya bilioni 279 katika kipindi kilichopita na mwaka
huu bilioni 3 zimetengwa katika Bajeti na zitaingizwa katika mfuko huu
ili uweze kutimiza majukumu yake kwa ufanishi na tumekuwa
tukiwashirikisha wadau katika kuchangia na wamekuwa wakituunga mkono na
tunaendelea kuwaomba wajitokeze zaidi kuchangia mfuko huu ” Alisisitiza Mhagama.
Akifafanua
Mhe. Mhagama alisema kuwa tayari mapendekezo kuhusu kuwepo kwa tozo
maalum katika kodi yameshawasilishwa katika kamati husika kwa hatua
zaidi dhamira ikiwa ni kuujengea mfuko huo uwezo wa kuwa na fedha za
kutosha katika kufanikisha vita dhidi ya Ukimwi hapa nchini.
Mkakati
mwingine ni ujenzi wa kituo maalum katika eneo la Mererani Mkoani
Manyara kitakachosaidia katika mapambano dhidi ya Ukimwi kwa kuwa eneo
hilo ni moja ya maeneo yenye mwingiliano mkubwa wa watu kutokana na
shughuli za uchimbaji madini.
Hatua
nyingine ni kufanya kazi kwa kushirikiana kati ya TACAIDS na Mamlaka
ya Kupambana na Dawa za Kulevya ili kuwafikia waathirika wa dawa za
kulevya ambao ni moja ya makundi yanayoathika na ugonjwa wa ukimwi kwa
mujibu wa tafiti mbalimbali.
Kwa
Upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Osca Mukasa (Mb) alisema
kuwa kutengwa kwa fedha katika bajeti ya 2018/19 zitakazopelekwa katika
mfuko wa kudhibi Ukimwi ni ishara nzuri kuwa serikali imeweka mkazo
katika mapambano dhidi ya janga hilo.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko alisema Tume hiyo
iko katika hatua za mwisho za kukamilisha mkakati wa Nne unaolenga
kuongeza nguvu ili kufikiwa kwa malengo ya mkakati huo.
Akifafanua
Dkt. Maboko alisema kuwa Tume hiyo imeandaa kampeni maalum kuhamasisha
wananchi kupima ili kujijua kama wameambikizwa virusi vya ukimwi au laa
hali itakayowasaidia kuchukua hatua stahiki na kwa wakati hivyo kuzuia
maambukizi mapya hasa kwa vijana.
“Hapa
nchini kwa mwaka kuna maambukizi mapya elfu 81,000 hivyo ni vyema
tukaungana katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu kwa kuwa uwezo wa
kuzuia maambuki mapya tunao”. Alisisitiza Dkt. Maboko.
Warsha
kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya
imefanyika mjini Dodoma leo ikiwashirikisha wajumbe wote wa kamati
hiyo, Aidha mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) unalenga
kuongeza rasilimali fedha kutoka asilimia 7 (2015) hadi asilimia 30
(2018).
0 comments:
Chapisha Maoni