Askofu
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick
Shoo ameonya kwamba asitokee kiongozi yeyote nchini wa kisiasa au
serikali ambaye atajaribu kuwazuia na kuwaziba midomo viongozi wa dini
kutekeleza wajibu wao wa kukemea na kuonya juu ya maovu yanayoendelea
hapa nchini.
Dk.
Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, pia amesema kamwe
kanisa halitanyamaza kimya kwa wanasiasa wenye tabia ya kutumia nafasi
zao kuligawa taifa vipande vipande.
Alizungumza
hayo jana kwenye ibada maalumu ya kusataafu kwa aliyekuwa Mchungaji wa
Usharika wa Masama Kati, John Mshau wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro.
“Wajibu
wa viongozi wa dini ni kuonya na kukemea yale mabaya yanayoendelea
nchini na si vinginevyo na kwamba asijaribu kutokea mtu yeyote kuwazuia
viongozi wa dini kufanya wajibu huo kwani ni sawa na kupingana na
Mungu.
“Wajibu
wetu ni kuonya, kushauri, kukemea na tunatenda hivyo, asijaribu kuja
mtu yeyote kutuzuia kufanya hivyo kwani neno la Mungu linasema bwana
hutegemeza wenye upole na huangusha chini wenye hila, hivyo sisi kama
viongozi wa dini hatutakubali kunyamaza tutasema na kukemea maovu,” amesema
Pamoja
na mambo mengine, Dk. Shoo aliwaonya viongozi wote wa kisiasa nchini
kuacha kutumia vyama vyao kuligawa taifa na kwamba suala hilo halitaweza
kuvumiliwa na viongozi wa dini na wataendelea kusema na kuonya.
Akitolea
ufafanuzi waraka ulioandaliwa na Baraza la Maaskofu 27 wa KKKT, Machi
15 Jijini Arusha alisema walifunga na kuomba Mungu kwa lengo la kupata
ujumbe sahihi ili wautoe kwa waumini wa kanisa hilo na Taifa kwa ujumla
na kwamba hawakukurupuka kutoa ujumbe huo.
0 comments:
Chapisha Maoni