Mwanamuziki
wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amemjibu msanii
mwenzake Amber Lulu ambaye wiki iliyopita alisema Ommy hana muonekano wa
kiume.
Kwenye
mahojiano aliyofanya na Jonijoo wiki iliyopita Amber aliulizwa kati ya
Jux na Ommy Dimpoz ni mwanaume yupi ambaye anaweza akawa naye kimapenzi
na moja kwa moja Amber Lulu alisema Jux kwa sababu Ommy hana muonekano
wa kiume
"Jux
sawa, Dimpoz hajakaa kama mwanaume, Ommy Dimpoz hawezi kukaa au
kushindana na Jux ni zero, hana mvuto wowote , hamna chochote
kinachonivutia kutoka kwake”.
Baada
ya video clip hiyo kutrend sana ambayo ilikuwa inamuonyesha Amber
akiongea hayo Ommy Dimpoz alijibu tuhuma hizo za Amber Lulu kuwa hana
mvuto na hana muonekano wa kiume ambapo ameweka nyeusi kwa kusema hataki
kumuongelea mtu huyo (Amber Lulu).
Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 Ommy Dimpoz alifunguka maneno haya:
"Mimi
sijui chochote na sijui hizo stori zimetoka wapi na zimeanzia wapi
lakini kikubwa sisi kama wasanii unajua kila siku vitu ambavyo
vinatuzunguka ni mambo ya mitandao, kwa hiyo in short no comment”.
0 comments:
Chapisha Maoni