Mwanyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) Hashim Rungwe ameliomba jeshi la polisi kusaidia upatikanaji wa Mpwa wake Saida Hilal (40) na mumewe Abdallah Kutiku ambao hawajaonekana tangu Machi 26, 2018 majira ya asubuhi.
Hashim Rungwe amesema hayo jana Machi 27, 2018 na kudai Saida Hilal aliaga wenzake ofisini na kwenda kituo cha polisi kufuatilia suala la mume wake Abdallah Kutiku ambaye alichukuliwa na polisi
"Huyu
binti alikuwa anafuatilia habari za mumewe polisi kwa kuwa mumewe
alikuwa amekamatwa na polisi hivyo naye hapatikani kwa hiyo wote wawili
hawaonekani kwani tulipofika kituo cha polisi walisema hawa watu
hatuwafahamu na wala hawajafika pale
"
Tangu hapo Bi. Saida Hilal hapatikani kwenye simu zake na tumefanya
jitihada kumtafuta kwenye vituo vya polisi na mahospitali kama
Muhimbili, Mwananyamala na sehemu zingine za usalama bila mafanikio.
"Sehemu
zote ambazo alikuwa anapenda kutembelea zote tumepita na
hatujafanikiwa, tunaomba vyombo vya dola watusaidie kuwatafuta hawa wote
na kama wanawashikilia kwa mujibu wa sheria tungeomba tufahamu ili
iweze kutuondolewa hofu kubwa tuliyonayo.
"Tunahofu
kubwa juu ya kutoonekana huyu binti maana ana watoto watano alitoka
asubuhi nyumbani kwake na kwenda kazini, yeye anafanya kazi Tume ya
Uchaguzi, kazini kwake haonekani na watu wa kazini wamejitahidi
kumtafuta wamekwama"
0 comments:
Chapisha Maoni