Ofisi
ya Mkuu wa Dar es Salaam ilitangaza kutoa msaada wa kisheria kwa
kuwasikiliza wanawake hao na kwamba watatoa msaada huo kwa siku tano
kuanzia Aprili mwaka huu.
Akizungumza
na wataalamu hao jana, Makonda alisema tatizo la wamama waliotelekezwa
ni kubwa na limekuwa likisababisha kinamama na watoto kuishi maisha ya
tabu na kusababisha ongezeko la watoto wa mitaani na vizazi vya watoto
wenye chuki na baba zao.
Makonda
alisema lengo la mchakato huo si ugomvi bali ni kumwezesha mtoto
kupata mahitaji ili aweze kuitumia vyema fursa ya elimu bure chini ya
Serikali ya awamu ya tano.
Pia alisema amewahimiza wataalamu hao kuhakikisha wanawasikiliza kinamama kwa umakini na kusimamia haki pasipo upendeleo.
Pamoja
na hayo Makonda alisema wapo kinababa ambao wameanza kutoa fedha ya
matunzo ya mtoto baana ya kusikia tangazo ambapo amewaomba kinamama
kufika Aprili 9 mwaka huu kwa ajili ya kuonana na watalaamu ili waingie
kwenye mfumo rasmi wa kimaandishi.
"Ifike hatua mwanaume ukimpa mwanamke ujauzito bila mpangilio aogope kama ilivyo kwenye ubakaji,"alisema Makonda.
0 comments:
Chapisha Maoni