Kiongozi
wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema chama chake siyo jukwaa sahihi la
kuisifia Serikali kama wanachama wengine wanavyodhani.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jumamosi, Zitto amesema wanachama wanaodhani
kama chama hicho ni jukwaa la kuisifia Serikali wajitathimini au
kuchukua hatua kama wenzao walivyofanya.
Zitto amesema hayo ikiwa ni siku chache tangu aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Samson Mwigamba na wenzake kumi kuhamia CCM.
“Tulimwita
Mwigamba katika kikao cha chama aje kutueleza kama tunakikuka misingi
ya chama lakini hakufika. Chama kinaheshimu mchango wa kila Mwana-ACT,
lakini tunawashauri wanaondoka wasiwashawishi wanachama wengine
kuondoka,”
“Chama
kimejiridhisha kwamba bado tunaendelea kusimamia misingi ikiwamo
uzalendo sanjari na kupigania haki za demokrasia,”amesema Zitto
Amesema wanafanya yote hayo wakiongozwa na utu na uadilifu.
“Chama
chetu kina ahadi tano ambazo ni kupambana na rushwa na ufisadi na
kamati ya uongozi imebaini kama haijatoka katika misingi yake kama
wengine wanaoondoka wanavyodai,”amesema Zitto.
Amesema bado wanaendelea kupambana na umasikini na hali ya maisha kwa Watanzania wote.
“Hatujawahi hata siku moja kwenda kinyume na misingi ya chama hiki kama watu wanavyodai.”
0 comments:
Chapisha Maoni