Taarifa
zilizotolewa na Mratibu wa Elimu Kata ya Mtenga, Hebron Mwafungo
zimeeleza kuwa mwalimu huyo amekutwa akiwa amekufa baada ya kujichinja
nyumbani kwake muda wa saa sita mchana leo Jumamosi.
Amesema
kuwa mwalimu huyo alikwenda kazini kwake na saa 5 asubuhi alirejea
nyumbani na hakumkuta mkewe na baada ya muda walipata taarifa kuwa
mwalimu huyo amekutwa amekufa baada ya kujichinja koromeo chumbani
kwake.
Amesema
kuwa mwalimu huyo alikua akiishi na mdogo wake nyumbani hapo na
alipofika alimtuma mdogo wake mbali kidogo ya nyumba hiyo na baada ya
kurudi aliona damu na baada ya kuchungulia chumbani alikuta kaka yake
amefariki dunia kwa kujichinja koromeo na kutoa taarifa kwenye uongozi
wa kijiji hicho.
Amesema
baada ya kumdodosa mdogo wa marehemu huyo alidai kuwa kaka yake siku
za nyuma alikua na mgogoro na mkewe lakini ulikwisha ila anahisi kitendo
cha mkewe kuondoka nyumbani na kwenda mjini Namanyere huenda jambo hilo
lilimkasirisha na kuchukua hatua hiyo ya kujichinja.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema chanzo cha kifo hicho
bado hakijajulikana lakini polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini
kilichomsibu mwalimu huyo kiasi cha kuchukua maamuzi ya kujiua kikatili
namna hiyo.
0 comments:
Chapisha Maoni