Shirika
la afya duniani (WHO) limemteua rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe kuwa
balozi wa kuunganisha vita ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza
barani Afrika.
Kuteuliwa
kwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 kumewashangaza wanachama wengi wa
shirika hilo pamoja na wafadhili hasa kutokana na hali ya sekta ya afya
nchini Zimbabwe.
Wanachama
wengi na wafadhili wa shirika la afya duniani wamedai kuwa chini ya
uongozi wa rais Mugabe sekta ya afya nchini Zimbabwe imezorota huku
wafanya kazi wakiwa hawalipwi ipasavyo na dawa pia hazitoshi jambo
ambalo linaonyesha kuwa Mugabe hakustahili kupewa wadhfa huo.
Upande
wa upinzani chini Zimbabwe umeuita uteuzi huo kuwa vichekesho na matusi
kwani kiongozi huyo ameshindwa kuhimarisha sekta ya afya nchini kwake
wakati yeye na familia yake wakitibiwa nje ya nchi.
Hata
hivyo kiongozi mpya wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus kutoka Ethiopia
ambaye ni mwafrika wa kwanza kuongoza shirika hilo alipongeza juhudi za
Zimbabwe kwa kujitoa kuboresha afya za wananchi.
0 comments:
Chapisha Maoni