Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mheshimia Azza Hilal Hamad kupitia
tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ametembelea Zahanati ya Solwa
iliyopo katika kijiji cha Solwa,kata ya Solwa,jimbo la Solwa mkoa wa
Shinyanga kisha kutoa msaada wa viti vya kisasa vya kujifungulia kwa
akina mama,vifaa vinavyotumika katika chumba cha kujifungulia na viti
vya wagonjwa (wheel chairs) vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi
milioni nne.
Vifaa hivyo ni miongoni mwa vifaa tiba alivyovipata kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania kwa lengo la kupunguza vifo vya mama na mtoto katika zahanati,vituo vya afya na hospitali mkoani Shinyanga.
Vifaa hivyo ni miongoni mwa vifaa tiba alivyovipata kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania kwa lengo la kupunguza vifo vya mama na mtoto katika zahanati,vituo vya afya na hospitali mkoani Shinyanga.
Akitoa msaada huo jana Alhamis May 11,2017 Mheshimiwa
Azza Hilal Hamad alisema msaada huo utasaidia katika kupunguza vifo
vinavyotokana na uzazi kwa kuwarahishia akina mama kupata huduma karibu
badala ya kutembea umbali kufuata huduma za afya.
“Mimi
ni mama nazifahamu changamoto wanazokabiliana nazo akina
mama,nilitafakari na kuangalia nani wa kuweza kutusaidia,nikaenda
ubalozi wa China nchini kuomba wasaidie akina mama wa
Shinyanga,walikubali na leo nimeleta vitanda vya kisasa kwa ajili ya
akina mama,viti vya wagonjwa na vifaa vinavyotumika katika chumba cha
kujifungulia”,alieleza Hamad.
Katika
hatua nyingine mbunge huyo aliwapongeza wananchi wa Solwa kwa kujitolea
na kuanza ujenzi wa jengo la wodi ya akina mama katika zahanati ya
Solwa ambapo ameahidi kuwapatia mabati 20 kwa ajili ya paa la jengo
hilo.
Aidha aliwataka wananchi kuachana na tabia ya kuwaozesha watoto wa kike
na badala yake wawatafutie shughuli zingine za kufanya wanapofeli
mtihani wa darasa la saba kwani wakiolewa wangali wadogo husababisha
wapoteze maisha wakati wa kujifungua hivyo kuchangia ongezeko la vifo
vya mama na mtoto katika jamii.
Mheshimiwa Hamad pia aliahidi kutafuta namna ya kumsaidia mtoto Salawa
Mihangwa (03) ambaye ana tatizo la ugonjwa wa moyo na amekuwa akilelewa
na kupatiwa huduma za kiafya katika zahanati hiyo baada ya mzazi wake
Grace Richard kukosa shilingi milioni 2.6 kwa ajili ya mtoto huyo
kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad, (CCM)
akizungumza na wananchi wa kijiji cha Solwa kata ya Solwa jimbo la Solwa
mkoani Shinyanga alipotembelea zahanati ya Solwa kisha kukabidhi msaada
wa viti viwili vya kisasa vya kujifungulia kwa akina mama,viti viwili
kwa ajili ya wagonjwa na vifaa vinavyotumika katika chumba cha
kujifungulia kwa akina mama
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad (CCM)
akizungumza wakati wa kumkabidhi Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Solwa
Dkt. Edwin Ibrahim (kulia) vifaa vinavyotumika katika chumba cha
kujifungulia akina mama (alivyoshikilia Dkt. Ibrahim )
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad (CCM)
akishikana mkono na mwenyekiti wa kijiji cha Solwa Emmanuel Ngamba
wakati akikabidhivitanda vya kujifungulia,viti vya wagonjwa na vifaa
vinavyotumika kwenye chumba cha kujifungulia akina mama
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad (CCM)
akionesha baadhi ya vifaa vinavyotumika katika chumba cha kujifungulia
Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Hellena Daudi akiwa na
baadhi ya madiwani wa CCM wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa tiba katika
zahanati ya Solwa
Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Angel Robert akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba katika zahanati ya Solwa
Diwani wa kata ya Solwa Shadrack Awadh akielezea matatizo yanayokabili wananchi wa kata hiyo
Wazee wa kata ya Solwa wakikabidhi zawadi ya mbuzi kwa mbunge Azza Hilal Hamad
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akifurahia jambo na wananchi wa kata ya Solwa baada ya kumaliza zoezi la kukabidhi vifaa tiba kwa ajili ya zahanati ya Solwa
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiteta jambo na mmoja wa wazee wanaoishi katika kata ya Solwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad
(CCM) akiwa amebeba mtoto katika chumba kinachotumika kama wodi ya
akina mama katika zahanati ya Solwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad
(CCM) akishiriki ujenzi wa jengo la wodi ya akina mama katika zahanati
ya Solwa ambapo aliahidi kutoa mabati 20 kusaidia ujenzi huo ambao
umetokana na nguvu za wananchi walioamua kuchangishana pesa na kuanza
kujenga ili kukabiliana na changamoto ya vifo vya akina mama na watoto
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad
(CCM) akishiriki ujenzi wa jengo la wodi ya akina mama katika zahanati
ya Solwa
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiweka
tofali wakati akishiriki ujenzi wa jengo la wodi ya akina mama zahanati
ya Solwa
Wa
pili kutoka kushoto ni mganga mfawidhi katika zahanati ya Solwa, Dkt.
Edwin Ibrahim akielezea kuhusu mradi wa Lishe wanaoutoa katika zahanati
hiyo kukabiliana na tatizo la utapiamlo kwa watoto lililokithiri katika
jimbo la Solwa. Dkt. Ibrahim alimweleza mbunge Azza Hilal Hamad kuwa
zahanati hiyo imekuwa ikitoa elimu ya lishe kwa akina mama na kutoa
chakula dawa kwa ajili ya watoto ambao hali zao kiafya siyo nzuri (wenye
utapiamlo)
Ndani ya chumba cha lishe-Mheshimiwa
Azza Hilal Hamad na diwani wa kata ya Solwa Shadrack Awadh wakiangalia
chakula dawa ( unga maalum wenye lishe) 'Multiple Micronutrient powder)
kinachotolewa kwa watoto wenye utapiamlo wanaofika katika zahanati ya
Solwa
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)
akiwa amembeba mtoto Salawa Mihangwa (03) ambaye ana tatizo la ugonjwa
wa moyo na amekuwa akilelewa katika zahanati ya Solwa baada ya mzazi
wake Grace Richard (kushoto) kukosa shilingi milioni 2.6 kwa ajili ya
mtoto huyo kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)
akimweleza mama wa mtoto huyo kuwa ameguswa na hali ya mtoto huyo ambaye
afya yake siyo nzuri hivyo kuahidi kutumia mbinu mbalimbali ili mtoto
aweze kufanyiwa huduma ya upasuaji
Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Solwa Dkt. Edwin Ibrahim akimwonesha
mheshimiwa Azza Hilal Hamad vyeti vya mtoto Salawa Mihangwa
anayesumbuliwa na ugonjwa wa moyo na amekuwa akilelewa katika zahanati
ya Solwa ambayo sasa inalea watoto 95 wenye tatizo la utapiamlo huku
mtoto anayesumbuliwa na ugonjwa wa moyo akiwa mtoto wa kwanza kulelewa
katika zahanati hiyo
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza na akina mama wenye watoto
wanaolelewa katika zahanati ya Solwa kutokana na watoto kukabiliwa na
utapiamlo ambapo aliwasisitiza kuwapatia watoto mlo kamili na kuzingatia
ushauri wanaopewa na wataalam wa masuala ya afya
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akigawa matunda kwa watoto wanaopata huduma ya lishe katika zahanati ya Solwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiondoka katika zahanati ya Solwa baada ya kukabidhi vifaa tiba vitakavyosaidia kupunguza vifo vya akina mama na watoto.