Idadi
ya wanajeshi na polisi waliouawa katika mapambano na wapiganaji wa
Kiislamu katika eneo la Bahariya magharibi mwa jangwa imefikia 53,
maofisa usalama na matabibu wamesema.
Wizara
ya mambo ya ndani imesema vikosi vya usalama vilikuwa vinawasaka
wapiganaji wa Kiislamu lakini waliviziwa katika chemchem ya maji ya
Bahariya umbali wa kilomita 200 kusini mashariki mwa Cairo na
kushambuliwa. Pia, imesema wapiganaji wa Kiislamu 15 wameuawa katika
makabiliano hayo.
Vyanzo
vilivyo karibu na maofisa usalama vinasema msafara huo ulishambuliwa
kwa roketi na wapiganaji hao pia walitumia vilipuzi. Duru za usalama
zinasema kuwa wapiganaji walikuwa na uelewa zaidi wa eneo hilo na ofisa
wa jeshi aliyetoa amri ya kuvamia alishindwa kuagiza wanajeshi
kuimarisha kikosi chake.
Hakuna
kikundi chochote kilichodai kuhusika ingawa kuna taarifa ambazo
hazijathibitishwa juu ya wapiganaji wa kikundi kinachofahamika kama
Hasm, kilichowahi kushambulia majeshi ya usalamasiku za nyuma. Hata
hivyo, Twitter ya kikundi hicho inayotumiwa mara kwa mara kutoa taarifa
haijafanya kazi tangu Oktoba 2.
Tangu
jeshi lilipomwondoa madarakani Rais Mohamed Morsi wa Muslim
Brotherhood, makundi ya kigaidi yameongeza sana mashambulizi yao dhidi
ya wanajeshi na polisi.
Brotherhood, waliowahi kuwa kundi kubwa la upinzani nchini wamekanusha kuhusu katika machafuko.
Mohamed
Morsi alichaguliwa kuwa rais mwaka 2012, lakini jeshi lilimpindua mwaka
mmoja baadaye baada ya kuibuka maandamano ya kupinga sheria ya Kiislamu
zinaosababisha mgawanyiko.
0 comments:
Chapisha Maoni