Jeshi
la Polisi mkoani Singida linamshikilia mganga wa kienyeji mkazi wa mtaa
wa Minga, Daud Idd (74), kwa tuhuma ya kunajisi watoto 14 wenye umri
kati ya miaka saba na 12 na kuwasababishia maumivu makali katika sehemu
zao za siri.
Mgonga
huyo maarufu kama Babu Karatu ameelezwa kuwa alikuwa akishirikiana
kutenda vitendo hivyo na mtoto wa mdogo wake aitwaye Abdallah Yahaya
(31).
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumamosi, kaimu kamanda wa
polisi mkoani hapa Isaya Mbughi amesema mtuhumiwa anadaiwa kutenda
makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Desemba mwaka jana, hadi Oktoba
mwaka huu.
Amesema
kuwa mwathirika mmoja mwenye umri wa miaka saba siku ya Oktoba 16 mwaka
huu saa 11.45 jioni wakati akiogeshwa na mama yake alilalamika kuwa
anasikia maumivu makali katika sehemu yake ya siri.
Amesema
baada ya binti kuyo kulalamika kwa mama yake mama huyo aliweza
kumchunguza kwenye sehemu zake za siri na kubaini kuwa michubuko
inayotokana na kuingiliwa kimwili.
“Mama
huyo baada ya kuona michubuko hiyo kwenye sehemu za siri za binti yake
alimhoji mtoto wake na mtoto huyo aliweza kumtaja mganga wa kienyeji
Karatu. Mwaathirika huyo alienda mbele zaidi na kumweleza mama yake kuwa
si yeye pekee hufanyiwa vitendo hivyo, bali wapo watoto wengi
wamefanyiwa.”
Kaimu
kamanda huyo amesema baada ya hapo mama huyo alitoa taarifa kwa
mwenyekiti wa mtaa wa Minga na kisha yeye na mwenyekiti wa mtaa waliweza
kuongozana hadi kituo cha kati cha polisi mjini hapa.
“Jeshi
la polisi liliweza kuwakamata watuhumiwa hao ambao wanaishi katika
nyumba moja, kwa tuhuma ya ubakaji. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa
watoto waliofanyiwa unyama huo wanasoma katika Shule za Msingi
Singidani, Nyerere na Mughanga,” amesema.
Mbughi
amesema mbinu iliyokuwa inatumika kuwanasa watoto hao wa ni kuwarubuni
na kisha kuwaonyesha video/movie, kwenye kompyuta mpakato.
“Wakati
watoto hao wa kike wakiendelea kuangalia video sebuleni, mtuhumiwa huyo
alikuwa akichomoa mmoja na kuingia naye chumbani na kumwingilia
kimwili. Wachache alikuwa akiwachezea sehemu zao za siri. Baada
kuingiliwa kimwili watoto hao walikuwa wakipewa zawadi ya shilingi mia
mbili au shilingi 2,000,” amesema.
0 comments:
Chapisha Maoni