Chama
cha Demokrasia na Maendeleo kimeweka wazi kwamba hakimuhitaji
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Bwana Christopher Kazeri kuwa
msimamizi wa uchaguzi mdogo kwa madai kwamba hawana imani naye pia hana
sifa kwani anaweza kusababisha umwagikaji wa damu.
Akiitoa
taarifa hiyo Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini Amani Golugwa amesema
kwamba Mkurugenzi huyo alipoteza sifa za kusimamia uchaguzi tangu Juni,
24 walipokuwa kwenye uchaguzi wa vitongoji na vijiji kwa kufoji
matokeo katika vijiji kadhaa na kuwalazimisha wasimamizi wabadilishe
namba kwenye fomu.
Golugwa
amesema kwamba vitendo ambavyo Mkurugenzi huyo alivifanya anavitafsiri
kama mambo ya kihuni kwani yalipelekea kugombanisha watu ambao ni ndugu
hivyo hofu yao ni kwamba anaweza kusababisha umwagikaji damu katika
uchaguzi mdogo wa marudiano Arumeru Mashariki.
"Tumeishauri
Tume iweze kuwasiliana na mamlaka ya uteuzi kwamba hatumtaki ndg Kazeri
awe msimamizi wa uchaguzi huu mdogo Arumeru Mashariki, kwanza
aliingilia uchaguzi wa vitongoji na vijiji na kulazimisha kubadilishwa
matokeo ambayo yalionyesha Chadema wameshinda, jambo ambalo lilileta
ugombanishi kwa wagombea, na hata wagombea wa CCM walikataa matokeo kwa
kukubali kwamba walishindwa na hata wasimamizi na askari waliokuwepo
hapo walithibitisha kwamba Chadema walikuwa wameshindwa" Golugwa
Ameongeza
"Kama uchaguzi wa vitongoji Mkurugenzi ametumia mabavu na kufanya uhuni
ambao tumeumbatanisha kwa Tume, kwenye uchaguzi huu wa madiwani si
ataleta hata vifaru au kusababisha umwagaji wa damu? Kwa busara na
hekima ya kawaida matendo aliyoyafanya Kazeri hayampi sifa ya kuwa
msimamizi.
Hata
hivyo Golugwa amefafanua na kusema kwamba wamewasilisha ushahidi wa
wagombea wa CCM wakikataa kupokea ushindi huo wa vitongoji kwa madai
kwamba hawawez kupokea ushindi wa mtutu wa bunduki.
0 comments:
Chapisha Maoni