Baaada
ya kimya cha muda mrefu Askofu Mkuu wa kanisa la ufufuo na uzima,
Mchungaji Josephat Gwajima ameibuka na kutangaza kuleta ndege aina ya
'Jet' Tanzania kwa ajili ya kutoa huduma kwa watumishi wake.
Mchungaji
Gwajima ambaye hivi sasa yupo mjini Birmingham, Alabama nchini Marekani
kwa shughuli zake za injili na mikutano mbalimbali ameahidi ataleta
ndege aina ya 'Jet'
"Muda si mrefu nitaleta Tanzania ndege hii 'Jet' kwa lengo la kukuza falme ya Mungu" alisema Gwajima
Mbali
na hilo Mchungaji Gwajima akiwa katika ziara zake hizo za kiroho alidai
kuwa amepata umeme megawati 250 kutoka nchini Ujerumani ambazo anaamini
zitasaidia taifa letu la Tanzania katika kukuza sekta ya viwanda.
"Nimepata
Umeme Megawati 250 kutoka Ujerumani kwa ajili ya Taifa letu katika
juhudi za kuunga mkono Tanzania ya Viwanda. Nilimtuma Engineer Mkuu wa
Ufufuo na Uzima Duniani Eng.Yeconia Bihagaze huko Ujerumani kufanya
ufuatiliaji, Umeme huu ni kwa ajili ya Watanzania wote na ujenzi wa
uchumi imara wa Tanzania ya Viwanda" alisema Mchungaji Gwajima
Hata hivyo mchungaji Gwajima aliwahi kuahidi pia ataleta treni la kisasa linalotumia Umeme Tanzania.
0 comments:
Chapisha Maoni