Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT), Sophia Simba, amesema hana mpango wa kukihama chama hicho.
Kauli
ya Simba imekuja baada ya kuwepo kwa tetesi zilizozagaa kwenye mitandao
ya kijamii kuwa ana mpango wa kukihama chama na kumfuata Waziri Mkuu
mstaafu, Edward Lowassa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Simba alisema hana mpango wa kukihama CCM
kwa sababu amelelewa na kukulia ndani ya chama hicho.
“Mimi
ni mwanachama wa CCM na pia ni mwenyekiti wa UWT, hivyo sina mpango
wowote wa kukihama chama changu na kile kinachozungumzwa ni uzushi,” alisema.
“Nafahamu kwamba CCM ndiyo iliyowezesha watu kunifahamu, naringa, natamba kwa sababu ya CCM.” Alisema amejipanga kuongoza timu ya wanawake wenzake ili kuhakikisha wanampeleka Dk. John Magufuli Ikulu.
“Tumevunja kambi zetu zote tumebaki na kambi moja tu ya tingatinga,” alisema.
Akizungumzia
kuhusu kuhama kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, alisema kila
mtu anahama chama kwa sababu zake na kwamba yeye (Simba) hana sababu ya
msingi ya kufanya hivyo.
“Slogan (kaulimbiu) yetu wanawake ni ‘wanawake jeshi kubwa, Magufuli ushindi ni lazima,” alisema.
Wakati
huo huo, akifungua Baraza Kuu Maalum la UWT, Simba alisema wawakilishi
watakaoshinda kwenye uchaguzi wanatakiwa kwenda kufanyakazi na si kwenda
kufanya maonyesho ya mavazi bungeni.
Pia, aliwataka wajumbe wa Baraza la UWT kuchagua wawakilishi wanaojiamini na watakaozungumza na kuwatetea wanawake bungeni.
Baraza la UWT limeanza vikao vyake jana kwa ajili ya kuwachagua wawakilishi na wabunge wa viti maalum.
0 comments:
Chapisha Maoni