Mbunge
wa jimbo la Tarime vijijini, kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) John Heche jana alikamatwa na polisi alipokwenda
kituo cha polisi cha Tarime kufuatilia kukamatwa kwa Katibu wake.
Mbunge
wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba amesema kuwa polisi walimkamata Heche
kutokana na kauli zake ikiwepo kauli ya kutaka kilimo cha bangi
kihalalishwe pamoja na kauli yake ya kuzuia shughuli za ACACIA.
"Mhe.
Heche alifika Polisi Tarime kwa ajili ya kufuatilia kukamatwa kwa
Katibu wake, katika hali ya kushangaza naye akawekwa chini ya ulinzi na
RCO na baadae kuelezwa kuwa alikuwa akitafutwa kwa makosa mawili
"Kosa
la kwanza ni Kauli aliyoitoa mapema mwaka huu katika mkutano wa
hadhara Sirari ya kwamba atapeleka hoja bungeni aiombe serikali
ihalalishe kilimo cha bangi na pili kauli yake ya hivi karibuni kuhusu
kuzuia shughuli za ACACIA Nyamongo kufuatia Kauli ya Rais kwamba mgodi
huo haupo kihalali nchini." alisema Marwa Ryoba
Aidha Mbunge Marwa anasema kuwa Heche alikataa kutoa maelezo yoyote polisi na jeshi la polisi limechukua simu zake zote
"Walimwachia
Heche ila wakachukua simu zake zote na kumtaka afike polisi Jumatatu
kwa mahojiano. Alikataa kuchukuliwa maelezo yoyote kwa kuwa hakuwa
amekwenda Polisi kwa mambo hayo bali kushughulikia kukamatwa kwa Katibu
wake, hivyo amejidhamini na kuondoka ila simu zimebaki Polisi" alisema Marwa Ryoba
0 comments:
Chapisha Maoni