Matamshi
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
kuhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kutoendelea na masomo yamezua gumzo
kubwa na mijadala mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Shirika
la wanawake barani Afrika limemtaka Rais Magufuli kuomba msamaha
kutokana na matamshi yake aliyoyatoa akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani
Pwani kuwa mwanafunzi atakayepata ujauzito katika utawala wake hataweza
kuendelea na masomo.
Hata
hivyo, katika sheria iliyopitishwa mwaka 2002 ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kuhusu suala la mtoto wa kike kupata ujauzito akiwa shule
inaruhusu kufukuzwa shule na kifungo cha miaka 30 kwa yule
aliyesababisha ujauzito huo.
0 comments:
Chapisha Maoni