Ulipomuuliza akaruka futi elfu 6 kwamba unamsingizia una kila ushahidi kwamba huyo jamaa ni kimeo ila kwa sababu akili yako ina ujibwa ulezi uliochanganywa na alizeti ukamsamehe, sasa leo amekuoa na tabia zilezile walizokuonya rafiki zako zimeendelea, unashinda unalia na kuimba Pambio la bwana tenda miujiza usiaache mpaka mwaka huu upite.
Alishatenda muujiza kukuonyesha ushahidi hukutaka kumsikia, ukapenda zaidi matarumbeta ya harusi bila kujali ndoa itakuwaje. Pole hakuna muujiza hapo, jipigie matarumbeta kwa kujitendea muujiza. Kamwe usidharau Mungu akikuonyesha (clear Signs) kwamba mtu uliyenaye ni shida. Using'ang'anie kuwa mjumbe wa bunge la katiba kama unahisi posho haitoshi achia ngazi.
Heri ukose harusi leo ujiandae kwa ndoa bora ya keshokutwa.