Waziri
wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amezionya taasisi zisizo za Serikali
zinazohamasisha kudai haki ya mtoto anayepata mimba kurejeshwa shuleni
kuacha mara moja na zikiendelea atazifutia usajili.
Mwigulu
ameyasema hayo leo, Jumapili wakati alipomwakilisha Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Parokia ya Kisasa Mjini
hapa.
Amesema Serikali haitaomba ushauri wala maoni kwa sababu maelezo yaliyotolewa na Rais, John Magufuli ni maagizo ya Serikali.
Waziri
huyo amesema Serikali imetoa haki ya kila mtoto kupata elimu kwa
kuifanya kuwa bure kwa hiyo atakayeikosa asitafute kisingizio.
"Rais
ametoa haki hiyo sasa hivi elimu ni bure, halipi tuition wala nini,
atakayeamua kuachana na haki hiyo asitafute kisingizio, asipeleke lawama
kwa Serikali, "amesema.
Loooo!!! Uhuru wa kufikiri na kutafakari kwa kina na kutofautiana na mtu YEYOTE na hatimaye kuwa na Naomi yako binafsi Uko wapi??
JibuFuta