Barrick
Gold Corporation yenye makao yake jijini Toronto, Canada, litaunda
kampuni mpya (sio Acacia) kuendesha migodi yake ya Bulyanhuru, Buzwagi
na North Mara nchini Tanzania.
Katika
taarifa yake juu ya makubaliano na serikali ya Tanzania yaliyofikiwa
juzi jijini Dar es salaam, Shirika hilo limesema msimamo wa uwazi
ulioafikiwa baina ya washirika (Tanzania na Barrick) ndio utaoainisha
namna kampuni hiyo mpya itafanya shughuli zake.
"Kwa
mfano Serikali ya Tanzania itashiriki katika maamuzi yahusuyo shughuli,
uwekezaji, mipango, manunuzi na masoko (ya kampuni hiyo mpya
itapoanzishwa)", sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Makamu wa Rais
Mwandamizi wa Barrick Gold anayeshughulikia Shughuli za Uwekezaji na
utawala Bw. Daniel Oh na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Barrick
anayeshughulikia Mawasiliano Bw. Andy Lloyd.
Taarifa
imesema kampuni hiyo mpya itaajili Watanzania, itawajengea uwezo
wazawa katika ngazi zote, kuanzia uanachama wa bodi hadi shughuli zote,
na kwamba itaongeza ununuzi wa bidhaa na huduma ndani ya Tanzania
katika kuhakikisha faida ya dhahabu inaifaidisha nchi.
Taarifa
hiyo imethibitisha kwamba faida ya kiuchumi kutoka katika migodi hiyo
mitatu itagawanwa nusu-kwa-nusu ama 50-kwa-50 baina ya kampuni hiyo mpya
na serikali ya Tanzania, faida yake ya kiuchumi ikitokana na mirahaba
na kodi huku asilimia 16 ikibakia pale pale.
0 comments:
Chapisha Maoni