Mwimbaji
TID aka Mnyama kama anavyopenda kuitwa, ametishia kutinga katika kituo
cha kati cha polisi jijini Dar es Salaam kuwasilisha malalamiko yake
dhidi ya Quick Rocka na kundi la OMG.
TID
ambaye ana historia ya kufikishwa yeye kwenye kituo ha polisi na hata
kufungwa miezi kadhaa, sasa amebadili upepo na yeye anahitaji haki yake
kisheria.
Kupitia
mtandao wa Instagram, Mnyama ametishia kufika polisi kuwasilisha
malalamiko yake kutokana na kile alichodai kundi la OMG na Bosi wao
Quick wametumia wimbo wake ‘Watasema’ bila ruhusa yake. Hivyo, anahitaji
kulipwa angalau milioni 20 kama kifuta jasho kwa kazi yake iliyowahi
kushinda tuzo mbili.
“Wat
is this….?! Hivi ndio mnapata Magari yenu!? @quickrocka &
@omgtanzania we need to TALK #Watasema, ameandia msanii huyo. Naomba
tukutane Central Police huwezi kutumia Haki zangu hivihivi Kabla
sijafanya kitu kibaya nahitaji million 20 compensation… This song ni
Awards mbili Za Kisima Music Awards 2005 inKenya u can’t just Steal it,
Unalala Ndani Leo.” ameandika TID.
‘Watasema’ ni hit ya miaka mingi iliyopita, ambapo TID alimshirikisha Naaziz, malkia wa michano kutoka Necessary Noise ya Kenya.
0 comments:
Chapisha Maoni