Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Job Ndugai amewakumbusha
wabunge wa vyama vya upinzani hasa vinavyounda UKAWA umuhimu wa jamii
kukaa pamoja, kujadiliana na kumaliza tofauti zao.
Ndugai
ambaye ni mmoja wa wabunge wa Bunge la 11 aliyasema hayo baada ya
baadhi ya wabunge hasa wa upinzani kususia futari aliyoiandaa siku ya
Jumanne kwa ajili ya wabunge wote. Kiongozi huyo wa juu wa mhimili huo
alisema kuwa licha ya jukumu zito la kujadili na kupitish bajeti ya
serikali ya 2017/2018, ushirikiano kwa jamii ni muhimu.
Jambo
hilo lilmfanya asiwe na raha na kuamua kuzungumzia ndani ya bunge kwa
upole kabisa ambapo alisema kuwa, baada ya kuhudhuria futari
iliyoandaliwa na Waziri Mkuu Jumatatu, na baada ya kuwepo tetesi za
kususia ya kwake alisema, amejifunza kuwa baadhi wamekatazana kuhudhuria
shughuli kama hizo.
“Lakini
nikajifunza kitu kimoja ambacho sikupenda kukisema, ila nikiseme hapa
kidogo. Kuna wenzetu wamekatazana rasmi kuhudhuria shughuli kama hizi.”
Ndugai
aliyasema hayo Jumanne wakati akihitimisha kipindi cha maswali na
majibu kabla ya kupisha mapumziko na kisha kupigiwa kura kwa bajeti ya
serikali.
"Bunge
linaendeshwa kwa mawasiliano ya namna mbalimbali baina ya wabunge na
uongozi. Endapo kuna jambo linakwaza na kusababisha watu wasipate
futari pamoja, ni vizuri wakae pamoja na kuondoa jambo hilo,"
alizungumza Ndugai.
Licha
ya kutoa tahadhari hiyo, Ndugai alisema kuwa wabunge hao wana uhuru wa
kufanya hivyo (kutohudhuria) kama wanaona ni sawasawa.
“Siyo
mwezi wa chuki na kubaguana. Niwakaribishe tena kwenye futari kwa
watakaoweza kufika. Watakaoshindwa In Sha Allah, kila la heri.
Tutaendelea kuwa pamoja mjengo huu huu,” alisema Spika Ndugai
akihitimisha nasaha zake.
0 comments:
Chapisha Maoni