Jeshi
la polisi mkoani Mwanza linawashikilia wanawake wawili katika matukio
mawili tofauti likiwemo la mwanamke mmoja kumuua mwanaye.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema katika tukio la kwanza,
mwanamke mmoja mkazi wa Kisiwa cha Nyamango, Kijiji cha Soswa katika
Tarafa ya Buchosa, Nyamisi Bahati (27) anashikiliwa na polisi
akituhumiwa kumuua mtoto wake, Sakimu Hassan mwenye umri wa miezi saba
kwa kumtupa ndani ya Ziwa Victoria.
Msangi
alisema tukio hilo lilitokea juzi saa moja usiku wakati mtuhumiwa
alipotoka nyumbani kwake kwenda kuwasalimia wazazi wake huku ikidaiwa
kuwa aliondoka akiwa na mtoto wake.
“Akiwa
nyumbani kwao ghafla alitoka nje akiwa na mtoto wake, ilionekana kama
anaenda kumbembeleza baada ya muda alirejea akiwa hana mtoto ndipo bibi
yake alipoanza kuhoji alipo mtoto,” alisema Msangi.
Alisema baada ya kumhoji zaidi, baadaye mtuhumiwa alikiri kumtupa ndani ya Ziwa Victoria.
Baada
ya bibi kupokea taarifa hiyo ilimshtua na kuanza kupiga kelele kuomba
msaada kwa watu ili waweze kusaidia kumuokoa mtoto huyo.
Kamanda
huyo aliendelea kueleza kuwa majirani waliokusanyika katika tukio hilo
walisaidia kutoa taarifa kituo cha polisi ambao nao walifika eneo hilo
na kuanza shughuli ya uokozi hadi walipofanikiwa kuupata mwili wa
marehemu.
Msangi
alisema uchunguzi wa awali umebainisha kuwa mtuhumiwa ana matatizo ya
akili ingawa bado wapo kwenye upelelezi na mahojiano kujua ukweli wa
jambo hilo.
Katika
tukio la pili, polisi wanamshikilia mkazi wa mtaa wa Malulu, Kata ya
Igogo wilayani Nyamagana, Ghati Chacha (36) kwa madai ya kukutwa na
pombe haramu ya gongo lita 23.
0 comments:
Chapisha Maoni