Dereva
na kondakta wa daladala zinazofanya safari ndani ya Manispaa ya Moshi
mkoani Kilimanjaro, Soweto–Mbuyuni wanatuhumiwa kumbaka abiria wao kwa
zamu na kumuumiza sehemu za siri.
Tukio
hilo lililotokea Juni 12 saa moja jioni maeneo ya Veta katika uchochoro
uliopo karibu na shule ya Northen Highland iliyo umbali wa mita 400
kutoka barabara ya lami.
Akielezea
tukio hilo, binti huyo mwenye umri wa miaka 20 alisema alitumwa na bosi
wake kwenda kununua mahitaji ya nyumbani Soko la Mbuyuni na kumuelekeza
kuwa akimaliza apande basi la Soweto sokoni hapo na ashukie mwisho
ambako angechukua bodaboda ya kumfikisha nyumbani.
“Nilipomuuliza
konda akaniambia ndiyo na nikampigia bodaboda ambaye nilipewa namba na
bosi wangu ili ampe maelekezo huyo kondakta sehemu ambayo watanishusha
ili yeye anichukue hapo na wakazungumza na baadaye akanirejeshea simu
yangu,” alisema msichana huyo.
Alisema baada ya hapo safari ya kutoka Mbuyuni kwenda Soweto ilianza.
“Kwa
kuwa nilikuwa mgeni, sikuelewa hata kituo kipi cha kushukia.
Niliendelea kukaa hadi nilipoona watu wote wameisha kwenye (Toyota)
Hiace, ndipo nikamuuliza konda kwa nini hanishushi akasema bado
sijafika,” alisema.
Anasema
alishangaa kuona dereva anaenda kuegesha gari uchochoroni na
aliposimama, kondakta akashuka, akidai anaenda kujisaidia. “Aliporudi
kwanye gari alifunga mlango na wakazima taa na kuanza kuniambia kuwa
wamenipenda kama ninataka kuwa hai nikubaliane na wanachokitaka na
nikikataa wataniua,” alisema binti huyo.
Alisema baadaye dereva alitoka kwenye usukani na kumfuata alipokaa na kuanza kumpapasa.
Alisema
alipoona hivyo alijaribu kutoka nje kupitia dirishani, lakini walimvuta
ndani huku wakimfunga mdomo asipige kelele na kumtishia kumuua.
“Nilikubali
yaishe na nikatulia. Akaanza dereva huku kondakta akinishika mikono na
baada ya kumaliza alichofanya, konda naye akaja akafanya hivyohivyo.
Nilisikia maumivu, lakini nilishindwa kupiga kelele kwa kuwa walinitisha
kuwa wangeniua,” alisema dada huyo.
“Walipomaliza
kufanya ukatili huo, konda alimwambia dereva kuwa waniue kwa kuwa
nimeshawatambua, lakini dereva akasema hakuna haja.”
Alisema
katika mabishano hayo alijikaza na kuwaambia kuwa yeye ni mgeni na
hajui popote kwa hiyo hatamwambia mtu kwa kuwa hilo ni tukio la aibu.
“Walikubaliana
na mimi na wakaniambia kuwa ni kweli kubakwa ni kitendo cha aibu kwa
hiyo nikimwambia mtu nitatengwa na jamii. Nikawaomba wanisaidie sehemu
ya kupata msaada niweze kufika nyumbani,” alisema.
Alisema
baadaye aliwaomba aende kuchukua kiatu chake kilichokuwa kimedondoka
dirishani wakati akitaka kuruka, na walipomruhusu akatumia nafasi hiyo
kusoma namba za gari.
Mlezi
wake, Abdi Massawe alisema baada ya kufika nyumbani akiwa na bodaboda,
binti huyo alimweleza tukio hilo na akatoa taarifa polisi ambako alipewa
fomu ya matibabu aliyoitumia Hospitali ya Mawenzi, ambako vipimo
vilithibitisha kuwa alibakwa.
“Huyu binti ni mgeni kutoka mkoani Singida. Hapa Moshi ana mwezi mmoja tu,” alisema Masssawe.
Massawe
alisema baada ya hapo alianza kusaka daladala hilo kwa kutumia namba
alizopewa na binti huyo na kufanikiwa kuikuta maeneo ya Soweto. Baadaye
aliwapigia simu polisi ambao walifika na kushusha abiria waliokuwamo na
kuipeleka kituoni.
Alisema wakati dereva akiendelea na mahojiano kondakta alitoroka.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita alisema derava wa
gari hilo aliyemtaja kuwa ni Salimu Abdalla (30) anashikiliwa na polisi
ambao wanaendelea kumtafuta kondakta ambaye alitoroka akiwa katika kituo
cha polisi.
Kwa sasa binti huyo anatibiwa Hospitali ya Mawenzi.
0 comments:
Chapisha Maoni