Katika
hali isiyokuwa ya kawaida iliyotokea jana Jijini Dar es salaam kwa
kitendo cha aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Fedha katika utawala wa
awamu ya nne, Adam Malima kutishiwa bunduki na askali mmoja aliyekuwa
doria kimewashangaza wengi na kupelekea Mbunge wa Kigoma Mjini, Zuberi
Zitto Kabwe kuonyesha masikitiko yake hadharani kwa kitendo
kilichofanywa na askali huyo.
Zitto
kabwe ameonyesha masikitiko hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii
Facebook akihoji kama polisi wanafundishwa kuwafanyia hivyo raia
wasiokuwa na hatia kiasi cha kuibua hofu katika jamii inayowazunguka na
kupoteza imani na jeshi hilo la polisi.
“Hii
ni nini ?, askari wetu wanafundishwa kufanya hivi, Waziri Mwigulu huyu
yupo wazi na ni wa kutoka kwako. Unahitaji uchunguzi”. Ameandika Zitto.
Zitto
aliandika hayo baada ya muda mchache kupita kwa tukio hilo
lililowahusisha askari hao walioambatana na kampuni ya Majembe Auction
Mart waliokuwa wakitaka kujaribu kukamata gari iliyokuwa imeegeshwa
pembeni ya barabara ya Masaki karibu na Hoteli ya Double tree ingawa
ndani ya gari hilo alikuwepo dereva.
0 comments:
Chapisha Maoni