Kamati
ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM),
imetengua uteuzi wa nafasi ya Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na
Chipukizi wa Umoja huo iliyokuwa ikiongozwa na Jokate Mwegelo .
Jokate aliteuliwa Aprili mwaka jana na Kamati hiyo kukaimu kwa muda kabla ya kamati hiyo kufanya uchaguzi.
Kaimu
Katibu Mkuu Taifa wa Umoja Shaka Hamdu amekiri Jokate kutenguliwa kwa
nafasi hiyo leo Machi 25, 2018 kupitia vikao vya Kamati vilivyokutana
kwa mujibu wa kanuni na taratibu za UVCCM.
“Kwanza
ifahamike Jokate aliteuliwa kukaimu kwa utaratibu wa UVCCM na
ameondolewa kwa utaratibu, ni kama alikuwa kwenye majaribio,” amesema
Shaka.
Shaka amesema utaratibu wa kujaza nafasi hiyo utafanyika hapo baadaye kupitia vikao vya umoja huo.
Uteuzi
wa Jokate kuwa Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipkizi,
ulionekana kutaka kuivuruga jumuiya hiyo baada ya kuibuka mjadala kwa
viongozi na wanachama wakidai uteuzi huo haukufuata kanuni na taratibu
za umoja huo.
0 comments:
Chapisha Maoni