Msanii
Afande Sele amefunguka mengine mapya kwa kudai shindano la Miss
Tanzania kwa sasa linatia aibu kubwa katika taifa kwa kukosa hadhi huku
likionekana ni shindano linalomnufainisha mtu mmoja nasiyo taifa kama
ilivyokuwa awali.
Afande
Sele amesema hayo baada ya watu wengi ndani na nje ya nchi
kutoridhishwa na zawadi ya gari aliyopewa Miss Tanzania 2016/2017, Diana
Edward wakidai limechakaa na linashusha hadhi ya mashindano hayo
pamoja na kuvunja moyo watu ambao walikuwa na lengo la kushiriki katika
mashindano mengine yajayo.
“Utapeli
ni nini ?....Gari ya Miss Tanzania 2017 na gari ya Miss Tanzania 2011
zinatoa jibu la swali hilo…Lakini pia ni vyema tukamuomba waziri husika
katika masuala hayo …a.k.a Dk. Marufuku akamuulize muandaaji wa Miss
Tanzania kama ni kweli ameaumua kuzeeka labda hata kufa na shindano
lake?”. Ameandika Afande Sele kupitia mtandao wake wa kijamii Instagram
Msanii huyo aliendelea kwa kusema
“Kama kweli iko hivyo basi itoshe pia kubadili jina la shindano kwa
kuliita Miss jina lake badala ya kuendelea kutia aibu Taifa kwa kuliita
Miss Tanzania huku likikosa hadhi ya kitaifa katika maeneo yote kwa
makusudi na maslahi yake yeye mtu mmoja tu…aibu yake aibu yetu…Imetosha
sasa…imestosha sana”.
0 comments:
Chapisha Maoni