Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema amewashangaa wanaomdhihaki na
kumshambulia kwa maneno makali mara baada ya kumpongeza mbunge wa
Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu kufuatia kuwasaidia majeruhi wa ajali
ya basi la Lucky Vicent.
Amesema
kuwa kwa hapa nchini kuwa mpinzani wa siasa za bongo ni kazi ngumu
sana, hivyo inahitaji kuwa na ujasiri wa kuweza kupambana ili uweze
kushindana na kila anayekushambulia hata kwa lile jema unalolifanya.
Baada
ya Mbunge Godbless Lema (Chadema) kumshukuru Mbunge wa Singida
Kaskazini (CCM) Lazaro Nyalandu kuna kundi la watu liliibuka na kuanza
kutoa maneno ya dhihaka kwa Lema huku wengine wakipongeza na kusema ni
jambo la kheri kwa mbunge huyo kutambua kazi iliyofanywa na Nyalandu,
lakini baada ya mijadala hiyo kuzidi kuwa mikuba Lema aliibuka na kutoa
kauli hii kuwajibu waliokuwa wakimdhihaki.
“Kuwa
mpinzani wa siasa Tanzania ni kazi ngumu sana, ila hatukati tamaa kwa
sababu upendo wetu ni mkuu kuliko dhihaka. Mungu awabariki” aliandika Godbless Lema
0 comments:
Chapisha Maoni