Baada ya hapo jana Msanii wa Bongo fleva na Hit maker wa wimbo wa Kidogo aliowashirikisha Mapacha kutoka Nigeria Peter na Paul Okoye Diamond Platnumz safari hii afanya kweli tena katika harakati za hapa na pale kuleta mabadiliko katika hili game la muziki kwa kuachia ngoma yake mpya aliyomshirikisha Rayvanny iliyopewa jina "SALOME".
Ngoma hiyo ambayo ina matoleo mawili tofauti moja likiwa na mahadhi ya kiasili na Nyingine ikiwa na midundo ya kuchezeka klabu. “Salome” imetungwa na mkali Diamond Platnumz pamoja na Rayvanny kutoka kwenye nyimbo halisi ya “Maria Salome” iliyoimbwa na mwana dada Saida Karoli.
Baada ya Kuachiwa kwa nyimbo hiyo na Video pia Mwana dada Saida Karoli ametoa pongezi na Kushukuru kwa Msanii DIamond kuiona nyimbo hiyo na kuamua kuifanya tena kwa stairi yake mwenyewe.
Ameandika hivi kupitia katika Akaunti yake ya Instagram..!!
UNAWEZA KUBOFYA HAPA KUITAZAMA VIDEO HIYO KAMA BADO HUJAITAZAMA