test

Jumanne, 20 Septemba 2016

Diamond kumjaza mapesa Saida Karoli, hiki ndicho atamlipa


Diamond amerudia baadhi ya vitu kwenye wimbo wake mpya ‘Salome’ aliomshirikisha Raymond kutoka kwenye wimbo wa ‘Maria Salome’ wa Saida Karoli uliotoka takribani miaka 16 iliyopita.

Akiongea na 255 ya Clouds FM Jumatatu hii, hitmaker huyo wa Kidogo amesema kuwa walizungumza na uongozi wa Saida Karoli na kumpatia kiasi cha fedha pamoja na asilimia 25 ya publishing ya wimbo huo.
“Kitu tulichokifanya kabla ya kurelease wimbo, tulizungumza na uongozi wake, tukawaambia tunafanya hiki na hiki na kuna kiasi pia tukakitoa ili kiende kwake halafu tukampa 25% ya publishing. Kila income ya publishing ikiwa inaingia katika huu wimbo, mama atakuwa anapata percent,” amesema Diamond.
Mpaka sasa video ya ‘Salome’ ya Diamond ina siku mbili tangu ilipoachiwa kwenye mtandao wa YouTube lakini imefanikiwa kutazamwa mara 659k.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx