Kesi
inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul
Nondo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa, imeahirishwa leo
(Jumatano).
Kesi hiyo imeahirishwa kutokana na hakimu kuwa na kesi nyingi na hivyo kuomba kupumzika.
Wakati
huo huo upande wa Jamhuri ulifika na mashahidi wanne kati ya watano
wanaotakiwa kutoa ushahidi huku mmoja akishindwa kufika mahakamani hapo.
Nondo
anashtakiwa kwa makosa mawili ikiwemo kuchapisha taarifa za uongo
mtandaoni March 7 ya mwaka huu kuwa maisha yake yapo hatarini akiwa
katika eneo la Ubungo na kuzisambaza kwenye mtandao wa Whatsapp.
Kosa
la pili limetajwa kuwa ni kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma
Mafinga wakati alipokuwa akitoa taarifa katika kituo cha polisi mjini
humo kwa kusema kuwa alitekwa na watu wasiojulikana.
0 comments:
Chapisha Maoni