test

Jumatano, 14 Septemba 2016

Mashahidi kesi ya Sh.bilioni 7 kutoa ushahidi leo


MASHAHIDI wawili katika kesi ya wizi wa utakatishaji fedha ya Sh bilioni saba inayowakabili waliokuwa wafanyakazi 13 wa Benki ya Exim jijini Arusha wanatarajia kutoa ushahidi wao leo katika mahakama ya wilaya ya Arusha na Arumeru mkoani Arusha.
“Septemba 14 mwaka huu tunatarajia kuleta mashahidi wawili ambao wako tayari kutoa ushahidi wao ''amesema Mwanasheria wa Serikali, Felix Kwetukia.

Awali shahidi wa 14 wa kesi hiyo, Hassani Kitundu (48) alimaliza kutoa ushahidi wake na aliieleza Mahakama kuwa alifanya biashara ya kupeleka watalii na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa kulipa dola za Kimarekani 5,000 katika Benki ya Exim Tawi la jijini Arusha na hakuwahi kusumbuliwa.
Kitundu ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya kitalii ya Expendition Tanzania, alisema hakuwahi kufanya biashara na mtu binafsi katika shughuli za kitalii kwa miaka yote aliyowahi kufanya kazi hiyo.
Watuhumiwa wa kesi hiyo kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2011 hadi 2012 wanatuhumiwa kuziibia kampuni mbalimbali za utalii jijini Arusha na NCAA kwa kufungua akaunti za dola za Kimarekani sita zenye majina tofauti, fedha za Kitanzania kwa kutumia mfumo wa malipo ya kadi na kufanikiwa kuchota kiasi hicho cha fedha.
Wakili wa serikali Kwetukia alidai baadhi ya wafanyakazi hao walikiri polisi wakati wakichukuliwa maelezo, lakini mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo ambaye alikuwa Meneja wa Tawi, Bimal Gondalia Gomes (34) alishtakiwa kwa kushindwa kuchukua hatua katika kipindi chote hicho wakati akiwa Meneja.
Watuhumiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ni pamoja na mshtakiwa wa kwanza Gomes anayatetewa na Wakili Adamu Jabir, Lilian Mgaya (33) anatetewa na mawakili wawili Anord Laizer na Philipo Mushi, mshitakiwa wa nne Livistone Julus (36) anatetewa na wakili Mosses Mahuna.
Mshitakiwa wa tano Joyce Kimaro (36)anatetewa na wakili Laizer na Mushi, mshtakiwa wa sita Daud Mosha anatetewa na wakili Johnes Mjema, mshitakiwa wa saba Doroth Tigana (50) anatetewa na wakili Edana Haraka, mshitakiwa wa nane Evans Kashebo (40) hana wakili, mshitakiwa wa kumi katika kesi hiyo Tuntufe Agrey (32) anatetewa na wakili Fediles Peter.
Mshtakiwa wa 11 katika kesi hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wakazi wa Jiji la Arusha ni Joseph Meck (34) hana wakili na mshtakiwa wa 12 Janes Massawe (32) anatetewa na mawakili Laizer na Mushi, mshitakiwa wa 13 Christophe Lyimo(34) anatetewa na wakili Laizer na Mushi.
Mshitakiwa wa 14 Gervas Gugo ambaye sio mfanyakazi wa Exim anatetewa na Laizer na Mushi na mshtakiwa wa 15 Deodet Chacha(35) anatetewa na Wakili Nafaniel Wantora.
Washitakiwa wanne ambao ni Gomes, mshtakiwa wa nane Kashebo, mshtakiwa wa 11 Neck na Lyimo wako nje kwa dhamana lakini washitakiwa wengine wote wako rumande kwa makosa ya utakatishaji fedha haramu kwani kesi hiyo haina dhamana kwa mujibu wa sheria.
Mshitakiwa wa tatu Neema Kinabo (30) na Mosses Chacha wamekiri makosa na kufanikiwa kulipa faini zaidi ya Sh milioni 230 na wameachiwa huru baada ya kulipa faini hiyo.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx