test

Jumapili, 10 Mei 2015

PICHA :>>>>>BASI LA DAR EXPRESS LIMETEKETEA KWA MOTO PWANI


Muonekano wa basi la Dar Express likiteketea kwa moto leo mchana eneo la Kwamakocho, Kijiji cha Kimange, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafari Ibrahimu amesema Basi la Dar Express lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Arusha, leo mchana limeteketea kwa moto eneo la Kwamakocho, Kijiji cha Kimange, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.Kamanda Ibrahimu amesema kuwa abiria wote waliokuwemo ndani ya basi hilo wako salama.
Eneo la Kwamakocho lipo katikati ya eneo la Mandela na Mbwewe mkoani Tanga.
RPC Jafari Ibrahimu amesema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na akasema uchunguzi unaendelea.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni