test

Jumanne, 1 Septemba 2015

Magufuli Atikisa Songea......Aweka shada la maua kwenye Kaburi la Marehemu Kapteni John Komba..




Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia  kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa majimaji mjini Songea jana ambapo mkutano huo ulihudhuriwa na maelfu ya wananchi mkoani humo.

 Akizungumza katika mkutano huo wakati akiomba kura Dr. John Pombe Magufuli aliwaambia wananchi hao kuwa  anataka kuijenga Tanzania mpya yenye viwanda vikubwa, vya kati na vya chini ili kuboresha uchumi wa nchi  na kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania na kuleta mabadiliko bora na siyo bora mabadiliko.
 
 Alisema pia serikali yake itaongeza kasi ya ujenzi wa barabara , Zahanati na Hospitali , kuongeza mafao ya wafanyakazi wa sekta mbalimbali ili kuongeza tija ya kazi , wanafunzi kusoma bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne nk.
 
 Alisema ataongeza zaidi  kasi yake katika utendaji  tofauti na alipokuwa  Waziri wa ujenzi kwani hapo awali alikuwa akiagizwa kama waziri na sasa  akichaguliwa na watanzania kuwa rais  yeye ndiye atakayeagiza na ole wake waziri atakayemteua asitekeleze maagizo yake atakiona cha moto.
 
 Dr John Pombe Magufuli pia alitembelea  na kuweka shada la maua  kwenye kaburi la Kada maarufu wa CCM marehemu Kapten John Damiano Komba ambaye alifariki  miezi kadhaa iliyopita jijini Dar es salaam katika hospitali ya jeshi Lugalo na kuzikwa nyumbani kwao huko Lituhi wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma ???????????????????????????????????? Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akitoa heshima katika kaburi la Kada maarufu wa CCM Marehemu John Damiano Komba katika kaburi lake huko Lituhi mkoani Ruvuma kulia ni Mjumba wa Kamti kuu ya CCM Ndugu William Lukuvi. ???????????????????????????????????? Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Kapteni John Komba huko Lituhi mkoani Ruvuma.

???????????????????????????????????? Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa kata ya Lituhi. ???????????????????????????????????? Umati wa wananchi ukiwa umefurika katika uwanja wa taifa mjini Mbinga katika mkutano wa kampeni uliohutubiwa na Dr. John Pombe Magufuli. ???????????????????????????????????? Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Mh William Lukuvi akiwapa salam za mikoa mingine ambako Dr. John Pombe Magufuli amepita. 15 Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa mjini Mbinga. 23 
Umati uliohudhuria katika mkutano huo 24 Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano huo uliofanyika Peramiho mkoani Ruvuma. 28 Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiingia kwenye uwanja wa Majimaji. 29 Majimaji ikiwa imetapika
37
Mwigulu Nchema akitema cheche kwenye uwanja wa majimaji

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni