Swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, CHADEMA, Leticia Nyerere
aliuliza endapo Serikali ina mpango wowote wa kuhalalisha matumizi ya
bangi kitabibu.
Mfano ulikuwa kutoka kwa Serikali ya Jimbo la DC nchini Marekani ambako
hivi majuzi walipitisha matumizi ya bangi kama dawa na kilevi!
Majibu ya naibu Waziri wa Afya yaliweka msisitizo kwenye uharamu wa
bangi kama isemavyo sheria ya Dawa za Kulevya ya mwaka 1971.
Pamoja na kufafanua matumizi ya kitabibu ya Bangi bado msimamo wa Serikali ulikuwa ni kuiacha nbangi kuwa haramu.
Ahsante Leticia kwa kujaribu!
SPIKA
wa Bunge, Anne Makinda amesema, bangi inayolimwa katika Mkoa wa Njombe
si kali kama inayolimwa mikoa mingine kutokana na baridi iliyopo
mkoani humo.
Makinda alijikuta akitoa jibu hilo huku akicheka kutokana na swali la
nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Christowaja Mtinda
(Chadema), ambaye alisema kuna baadhi ya maeneo nchini ukiwemo Mkoa wa
Njombe na Mara, mmea wa bangi umekuwa ukiota bila kupandwa na hutumika
kama chakula.
“Njombe bangi haioti yenyewe, tulikuwa tunapanda, lakini baada ya sheria
iliyopitishwa mwaka 1975, tuliacha kupanda bangi, lakini hata hivyo
bangi ya Njombe si kali kwa sababu ya baridi,” alisema Spika Makinda
huku akiwaacha wabunge na wageni wengine wakicheka.
Katika swali hilo, Mtinda aliitaka Serikali kufanya utafiti ili mmea huo uweze kutumika kama dawa.
Hata hivyo, akijibu kwa Niaba ya Waziri wa Afya, Naibu Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia alisema Serikali haipo
tayari kuhalalisha matumizi ya bangi kama dawa kwa sababu athari zake
ni nyingi kuliko faida.
Awali, katika swali la msingi Mbunge wa Viti Maalumu, Leticia Nyerere
(Chadema), alitaka kujua kuhusu msimamo wa Serikali kuhalalisha matumzi
ya bangi kama dawa kama ilivyofanya Serikali ya Columbia iliyoruhusu
matumizi ya bangi kwa ajili ya dawa.
Akijibu Nkamia alisema, msimamo wa Serikali ni kwamba inafuata sheria
inayoeleza kwa kina mtu yeyote atakayejihusisha na kutumia, kuhamasisha
matumizi, kuuza, kusafirisha, kuhifadhi au kujihusisha kwa namna
yoyote ile na bangi ni kosa la jinai.
“Adhabu ya makosa hayo ni kufikia hadi kifungo cha maisha. Napenda
kushauri na kusisitiza bangi ni miongoni mwa dawa za kulevya ambazo
tusizizalishe wala kuzisambaza kwa sababu madhara yake ni makubwa kwa
afya ya binadamu,” alisema Nkamia.
Source : JamboLeo
Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
xxxxxxxxxxxxx
0 comments:
Chapisha Maoni