test

Alhamisi, 3 Novemba 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 83 & 84 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )


MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
"KAMA MIMI SIJAKUWEKA, TUMBONI MWAÑGU MIEZI TISA, HUTO MUOA SHEILA, ILA KAMA NILIKUZA KWA UCHUNGU, BASI UTAMUOÀ SHEILA."
"HICHO KIBESI CHAKO WAPANDISHIE HAO WASICHANA WAKO, ILA SI MIMI MAMA YAKO. USIPO ANGALIA NITAMPOTEZA HUYO MBWA WAKO NA KITOTO CHAKE"
Mama alizungumza na kupiga hatua tatu mbele akanigeukia na kwaishara ya kidole chake, akaniamrisha nitangulie kwenye gari, huku yeye na mlinzi wake wakifwatia nyuma.

ENDELEA
   Katika siku ambayo nimejisikia vibaya ndani ya moyo wangu ni siku ya leo, sikutegemea kama mama yangu anaweza kumkataa mwanangu mbele yangu japo sijamuona, ila muonekano wa kwenye picha una dhihirisha kwamba Junio ni mwanangu wa damu. Kila nilipo mtazama aliye keti, pembeni ya siti yangu. Moyo ukazidi kuniuma, kiasi cha kutamani nishuke ndani ya gari, nitembee hata kwa miguu kurudi nyumbani.

Tukaafika nyumbani nikawa wa kwanza kushuka ndani ya gari. Sikuelea chumbani kwangu kuepusha kelele za Sheila, ambaye muda wote, mama anamchukulia Sheila kama mtoto mdogo. Chochote anacho kihitaji anakipata.
"Shem, mbona umekaa huku bustanini, peke yako”
Sauti ya ndugu wa Sheila anaye itwa Blanka, niliisikia ikinisemesha, nyuma yangu

"Hapana nina punga punga upepo"
"Ahaaa, basi nilijua kwamba hjarudi na mama"
"Nimerudi"
Blanka akakaa pembeni yangu, huku akivua viatu vyake na kuvisogeza pembeni
"Shem mbona kama, haupo sawa, unaumwa?"
Nikatingisha kichwa kumjibu Blanka
"Sasa n nini tatizo shem wangu? Sasa hivi ulitakiwa uwe ndani unafuraha"
"Hapana, nina furaha"
"Shem huna furaha, au dada amekudhi?"
"Hapana, kuna maswala yangu yakibiashara kidogo ndio ninayafikiria"
"Ahaaaa, ila shem kuna kitu nahitaji kukuuliza"
"Kitu gani?"
"Unampenda kweli dada Sheila?"
Ikabidi nimtazame Blank vizuri machoni mwake.
"Mbona umeniuliza hivyo?"
"Yaa nàhitaji kujua, kwa maana kuna vitu hapa nyuma vilikua vinaendelea"
"Sijakuelewa, vitu gani vilikua vinaendelea?"
"Kuna mambo alikua anayafanya dada Sheila, kwa upande wangu sijayapenda isitoshe anakwenda kufunga ndoa na wewe, sizani kama anastahili kua mkeo"
Moyo ukaanza kunienda mbio, nikamgeukia vizuri Blanka, kabla sijamuuliza kitu, nikamuona mama akija sehemu tulipo.

"Ina bidi uongeze juhudi kwenye masomo, isitoshe unasoma masomo ya udaktari, ujitahidi sana"
Ilinibidi kubadilisha mada, ili mama asielewe ni kitu gani tunazungumza. Chakumshukuru Mungu Blanka alinielewa maana yangu ya kubadili mada tuliyo kua tukiizungumza.
"B wezako wanakutafuta kule ndani"
"Ahaa sawa mama"
Blanka akanyanyuka na kuondoka, mama akakaa sehemu nilipo. Ukimya wa sekunde kadhaa ukakatiza, sikua na kitu cha kuzungumza.
"Hivi Eddy, ni nani aliye kuroga?"
"Hakuna"
"Nimempigia mchungaji simu, aje kukuombea"
"Ili iweje"
"Eddy wewe si bure, utakua umerogwa"
"Mama na elimu yako hiyo yote yaani una amini kwamba mimi nimerogwa?"
"Tena sana, na aliye kuroga amesha fariki"
Laiti kama añgekua si mama yangu, aliye nibeba tumboni mwake miezi tisa, ningemtandika ngumi, ambayo asinge isahau maisha yake yote.

"Na kama nilivyo kuambia, mtoto uliye naye mimi simtambui, na huyo mama yake naye simtambui. Sasa ole wako unidhalilishe kwa wageni nilio waalika. Haki ya Mungu naapa nitakuachia laana."
Mamà akanyanyuka, nakujifunga tenge lake vizuri.
"Na sitaki siku hata moja huyo mwanangu Sheila ajue, kwamba unamtoto. Akijua na kuchukua maamuzi mabaya utajuta"
Mama àkaondoka na kuniacha nikibaki nikimsindikiza kwa macho, yaliyo jaa hasira.
Kitu kilicho anza kuniumiza kichwa, nikuhitaji kujua ni mambo gani aliyo kua akiyafanya Sheila, kipindi ambacho mimi sikuwwepo. Nikaanza kuamini kwamba Blanka atakua ni msaada mkubwa sana kwangu.

Usiku sikuamini kumuona mchungaji akiwa ameketi kwenye sofa za sebleni, akizungumza na mama. Wakaniita, nikajumuika nao kwenye mazungumzo, mimi na mchungaji tukaingia kwenye chumba cha maombi, kilichopo ndani ya hili jumba jipya la mama.
  Bila hata mchungaji kuniuliza swali, lolote akaanza kuniombea huku akiuweka mkono wake juu ya kichwa changu
"Pepo mchafu uliyopo ndani ya kichwa cha huyu kijana toka kwà jina la Yesu kristo"
Mchungaji aliendelea kuniombea huku akinisukuma sukuma kichwa changu. Zaidi ya nusu saa mchungaji aliendelea kunisalia
”Mchungaji, nimechoka kupiga magoti kama mapepo sina si tuachane na hii biashara bwana"
"Ohhhh shagara bagharaa, pepo wewe mchafu huwezi jibizana na mimi mtu wa Mungu, hapo ulipo toka kwa jina la Yesu"

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx