Wakati
Chadema ikiendelea na mchakato wa kuwapata viongozi wake katika ngazi za
nchini, nafasi ya mwenyekiti imeonekana kuwa ni mwiba na ndiyo inayozungumzwa
ndani na nje ya chama hicho.
Mwanzoni
mwa mwaka huu, chama hicho kilitangaza kuanza kwa uchaguzi kulingana na kalenda
yake kuanzia ngazi ya Msingi hadi Taifa, lakini wakati chaguzi hizo zikiendelea
katika ngazi za awali za misingi, matawi na kata minong’ono imeibuka kwamba
kuna wanachama wanaotaka mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ang’atuke
madarakani.
Kulingana
na minong’ono hiyo, Mbowe anatakiwa ang’atuke apishe wengine kukiongoza chama
hicho kikuu cha upinzani nchini, huku nyingine ikitaka aendelee na uongozi kwa
kuwa hakuna mbadala wake.
Mbowe
aliyeanza kukiongoza chama hicho mwaka 2004 akichukua kijiti kutoka kwa Bob
Makani, anaelezwa kukijenga chama hicho ikiwamo kukiongoza kupata madiwani na
wabunge wengi.
Chini
ya uongozi wake kwa sasa Chadema ndiyo chama cha upinzani kinachoinyima CCM
usingizi, chenye wabunge wengi na idadi kubwa ya madiwani ukilinganishwa na
vyama vingine, ukiondoa chama tawala.
Kutokana
na idadi kubwa ya madiwani chama hicho kimeweza kuongoza halmashauri nyingi
ikiwamo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Upande
wanaotaka Mbowe aendelee wana hoja kwamba, kwa sasa ndani ya chama hicho hakuna
mbadala, labda kwa siku za usoni na wasingependa kuona aking’atuka kwa kuwa
hakuna wa kumuachia kijiti hicho cha uongozi.
Vilevile,
wanaitazama minong’ono ya kumpinga Mbowe kama imechagizwa na wapinzani wake nje
ya chama.
Mkurugenzi
wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema anasema ndani ya
chama hawana taarifa za mtu yeyote aliyeonyesha nia ya kugombea uongozi nafasi
ya juu ya chama hicho.
Wachambuzi
wa masuala ya siasa wanalitazama jina la Mbowe kama ndilo limeubeba uchaguzi
ndani ya Chadema na linazungumzwa licha ya kwamba uchaguzi bado uko hatua za
chini.
Pengine
bila jina la Mbowe au nafasi yake kutajwa, uchaguzi wa Chadema ungeendelea
kimyakimya kwa kuwa hakuna msisimko uliokuwa wazi.
Hata
hivyo, sehemu kubwa ya wana Chadema, na hasa viongozi wanaamini kwamba lengo la
minong’ono hiyo kuhusu mshikemshike juu ya uenyekiti ni kuwavuruga.
Mbowe na Ferguson
Naibu
Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu anasema kuwa kitu kizuri ni kwamba
wanajua kwamba wapo watu wenye nia ovu ya kutaka kuwavuruga lakini kamwe
hawatawapa nafasi hiyo.
Mwalimu
anasema kwake yeye, anaamini kwamba hakuna ubaya wowote kwa Mbowe kuendelea kubaki
katika nafasi hiyo kwa kuwa bado anatosha.
Anatoa
mfano wa timu ya mpira wa miguu ya Manchester United ya Uingereza ambayo baada
ya kufanya vizuri na kunyakua vikombe vitatu, mashabiki walimtaka kocha wake
wakati huo, Sir Alexander Ferguson kuachia ngazi na kumpisha mwingine kwa kile
walichodai kuwa hakuwa na jipya tena.
“Lakini
kila mtu leo ni shahidi nini kimetokea baada ya Ferguson kuondoka katika timu
ile; washabiki na wanaofuatilia mpira wanajua kilichotokea, Manchester United
iliporomoka na mpaka leo haijasimama vizuri kwa kuwa kocha huyo hakuondoka kwa
muda muafaka.
Kwa
mujibu wa Mwalimu, kwa sasa hakuna kijana ambaye yuko tayari kuchukua kijiti
cha Mbowe, ingawa pia anaamini kwamba kiongozi huyo hawezi kuongoza milele
kwani hata mwenyewe analijua hilo.
“Huwezi
kubadili mwenyekiti tu kama unavyoamua kubadili runinga yako nyumbani;
mwenyekiti ni taasisi na ni lazima ujiridhishe kwamba atakayebadilishwa ana
mlengo gani na chama, hilo ndiyo la msingi, tusije kuweka kirusi mwisho wa siku
kikawa mwiba kwa chama,” anasisitiza Mwalimu.
Hata
hivyo, Mwalimu anasema huwezi kumfananisha Mbowe na wenyeviti wengine wa vyama
vya upinzani ambao wanang’ang’ania madaraka, kwa kuwa yeye ni tofauti kutokana
na utendaji wake wa kuwaandaa vijana wasimame wenyewe.
“Ndiyo
maana leo unakuta Chadema kuna vijana weye uwezo ambao wameandaliwa vema kama
Halima Mdee, John Mrema, John Mnyika, Salumu Mwalimu, John Heche na wengine
wengi kwa sababu chama chetu kinatoa nafasi kwa kila mmoja,” anaongeza Mwalimu.
Hata
hivyo, Mwalimu anasema kuwa katika kuandaa huko vijana wapo waliopewa nafasi na
matokeo yake wakageuka wasaliti kisha kuanza chokochoko za kutaka kukidhoofisha
chama.
“Sisi
sote ni mashahidi, wapo vijana waliopewa nafasi na uongozi wa chama wakaonekana
na kuwa wakubwa lakini matokeo yake wakageuka wasaliti na kutaka
kukisambaratisha chama lakini waliishia kufukuzwa na chama kikaendelea kwa
sababu hakuna aliye mkubwa zaidi ya chama,” anasisitiza Mwalimu bila kutaja
vijana hao.
“Lazima
uwe na mpango maalumu na si leo unaamka unasema mwenyekiti hafai, kwanza katiba
yetu haijaweka ukomo; ni kweli kama binadamu mwenyekiti ana makosa na mapungufu
yake na siyo malaika, lakini lazima tuwe makini kwa kumuweka mtu sahihi
atakayekuwa msaada kwa chama na si ndumilakuwili,” anasisitiza.
Profesa Baregu atia neno
Akizungumzia
hilo Profesa wa sayansi ya siasa nchini, Mwesiga Baregu anasema suala la
kuendelea au kutoendelea kwa Mbowe ni la wanachama wenyewe na chama chao na si
vinginevyo.
Anasema
kuwa katiba ya chama hicho haijatoa ukomo wa mwenyekiti kugombea vipindi
vingapi hivyo kama wanachama na chama chao wataona anastahili kuendelea, hakuna
mtu wa kuwapinga kwa kuwa wao ndiyo wenye madaraka.
“Hiyo
minong’ono ni hisia tu, nadhani tuwaachie wenyewe wenye chama chao waamue
wanataka nini na sisi tufuate kwa kuwa hatuna tunachoweza kubadili,” anaongeza
Profesa Baregu.
Hata
hivyo, Profesa Baregu anasema jambo lingine linalosababisha minong’ono hiyo ni
fitina kutoka kwa wapinzani wa chama hicho ili kukidhoofisha.
“Sasa
kuna fitina sana. Mfano tumeona kilichotokea katika uchaguzi wa marudio katika
jimbo la Kinondoni, hivyo uwezekano wa watu wafitini kutumia nafasi ya uchaguzi
wa ndani kwa lengo la kuwasambaratisha ni mkubwa,” anaongeza.
Anasema
wafitini hao wana lengo la kuleta mgawanyiko na endapo hicho hakitagundua
mapema kitakwenda mrama.
“Mimi
sitarajii Chadema leo kuachwa bila kudhoofishwa, imepitia mengi na yaliyotekea
Kinondoni kwenye uchaguzi mdogo yanaleta funzo kubwa,” anaongeza Profesa
Baregu.
Profesa
Baregu anasema kwa sasa chama hicho kinapaswa kuwa macho na kisiamini mtu au
kitu chochote hasa kipindi hichi kinapoelekea katika uchaguzi wa ngazi
mbalimbali mpaka Taifa.
Hata
hivyo, Profesa Baregu anasema kuwa hali hiyo ni kawaida katika siasa za vyama
vingi na kwamba anaamini chama hicho kitavuka salama kama ilivyokuwa katika
vipindi vingine vya uchaguzi.
“Wote
ni mashahidi, misukosuko katika chaguzi za Chadema ni hali ya kawaida lakini
mwisho wa siku mambo yanasonga. Kinachopaswa ni umakini wa hali ya juu ili
kuvuka na kuendelea na maisha kama kawaida,” anaongeza.
Hatua za uchaguzi
Wakati
Profesa Baregu akisema hayo, Mrema anasema; “Chadema kwa sasa kimeelekeza nguvu
kubwa kwa uchaguzi wa ngazi za chini (msingi, matawi na mashina) na kwamba
baada ya hatua hiyo kukamilika watafuata nyingine.
Kwa
mujibu wa Mrema, tayari viongozi wakuu akiwamo Mbowe wanashiriki kikamilifu
katika mchakato huu na kwamba wataendelea kushiriki mpaka pale itakapofikia
hatua ya kitaifa.
Mwanachi
0 comments:
Chapisha Maoni