Rais
John Magufuli jana alikutana ana kwa ana na rafiki yake, Charles
Kitwanga ikiwa ni siku 80 baada ya kumvua cheo cha Waziri wa Mambo ya
Ndani kwa kosa la kuingia bungeni kujibu maswali akiwa amelewa.
Wawili hao walikutana kwenye Jimbo la Misungwi ambako Rais alisimama akitokea Wilaya ya Sengerema ambako alihutubia wananchi.
Rais alitengua uteuzi wa Kitwanga Mei 20, wakati sakata la utekelezwaji mbovu wa mkataba wa Sh37 bilioni baina ya Jeshi la Polisi na kampuni ya Lugumi Enterprises likivuma kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Lakini
jana, hali ilionekana ya kikazi zaidi wakati Rais alipofika kwenye
jimbo hilo. Kitwanga, ambaye ni mbunge wa Misungwi mkoani Mwanza, alitumia nafasi hiyo kukutana na Rais kwa mara ya kwanza hadharani, kuwasilisha kero za wananchi wake, hasa ya maji.
Katika
tukio hilo lililovutia hisia za waliokuwepo, Rais aliuthibitishia umma
kuwa yeye na Kitwanga ni marafiki wa muda mrefu, alipokuwa akijibu ombi
la mbunge huyo la kutaka Serikali itatue kero ya maji eneo la Usagara na
Misungwi.
“Kitwanga
ni rafiki yangu. Tayari Serikali imepanga kutumia zaidi ya Sh8 bilioni
kutekeleza mradi mkubwa wa maji maeneo ya jimbo la Misungwi, ikiwemo
Usagara,” alisema Rais Magufuli akiwa amesimama kwenye gari lililofunuliwa upande wa juu.
Katika
sakata la Lugumi, wabunge walitaka suala lijadiliwe baada ya taarifa ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kubaini kuwa
kampuni hiyo ilishindwa kufunga mashine za kielektroniki za kuchukulia
alama vidole kwa mujibu wa mkataba.
Mkataba
huo ulisainiwa mwaka 2011 lakini hadi CAG alipokuwa akifanya ukaguzi
mwaka jana, ni vituo 14 tu kati ya 118 vilivyokuwa vimefungwa mashine
hizo, huku Lugumi Enterprises ikiwa imelipwa Sh36 bilioni ambazo ni
zaidi ya asilimia 90 ya fedha za mkataba huo.
Kitwanga
alihusishwa na sakata hilo kutokana na dhamana yake na pia kuwa na hisa
kwenye kampuni ya Infosys, ambayo ni wakala wa kampuni ya Dell
inayozalisha kompyuta, kuhusishwa kutoa vifaa hivyo.
Hata hivyo, Juni 22, Kitwanga aliwaambia waandishi wa habari nyumbani kwake kuwa Infosys haina uhusiano wowote wa kibiashara na Lugumi.
Hata hivyo, Juni 22, Kitwanga aliwaambia waandishi wa habari nyumbani kwake kuwa Infosys haina uhusiano wowote wa kibiashara na Lugumi.
Jitihada
za wabunge, hasa wa upinzani kutaka kuzungumzia suala hilo zilikwama
kwa maelezo ya kutaka kusubiri ripoti ya kamati ndogo iliyoundwa
kuchunguza suala hilo.
Ripoti hiyo iliwasilishwa mwishoni mwa vikao vya Bunge la Bajeti na haikujadiliwa baada ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kusoma maagizo ya Bunge kwa pande zinazohusika kwenye mkataba.
Ripoti hiyo iliwasilishwa mwishoni mwa vikao vya Bunge la Bajeti na haikujadiliwa baada ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kusoma maagizo ya Bunge kwa pande zinazohusika kwenye mkataba.
Kabla
ya suala hilo kuzuiwa kujadiliwa, wabunge walikuwa wakidai kuwa Rais na
Kitwanga ni marafiki wa karibu na baadaye mitandao ya kijamii
ikasambaza mkanda unaoonyesha jinsi walivyokuwa wakijadili suala la
Magufuli kuchukua fomu ya kugombea urais.
Kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Magufuli alimnadi Kitwanga kwa kueleza kuwa anamfahamu kwa kuwa walisoma wote na ni rafiki yake.
Kabla ya kwenda Sengerema kwa kivuko jana, Rais alihutubia wilayani Sengerema ambako aliendelea na onyo lake dhidi ya watu anaosema wanataka kuvuruga amani.

Akihutubia
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mnadani mjini
Sengerema, Rais Magufuli aliwataka wenye lengo la kuvuruga amani
kumsubiri amalize kipindi chake cha uongozi kwa sababu hatawapa fursa
hiyo.
“Wapo wanaotumia taasisi za kisiasa na kidini kujaribu kuvuruga amani ya nchi. Hawa hatutawapa fursa hata kidogo kwa sababu amani ya nchi ikivurugika hakuna hata mmoja atakayebaki salama; sote tutaangamia,” alisema Rais Magufuli
Aliwakumbusha wakazi wa Sengerema jinsi walivyowapokea wakimbizi kutoka nchi jirani ya Rwanda miaka ya tisini wakati taifa hilo lilipoingia kwenye mauaji ya kimbari yaliyoishia kwa watu zaidi ya milioni moja kupoteza maisha.

“Tunayo
mifano hai ya mataifa yaliyochezea amani na kusambaratika. Rwanda
ilipitia njia hiyo kabla ya kusimama upya.Zipo Libya na Somalia ambazo
hadi sasa zimegawanyika vipande vipande,” alisema Rais Magufuli.
Aliwataka Watanzania kulinda kwa udi na uvumba amani na utulivu ulioasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na viongozi wengine, kwa kuwapiga vita wanaovuruga amani hata kama ni ndugu, jamaa, marafiki, wanachama au waumini wenzao.

anaendelea kutoa onyo hilo wakati Chadema ikiendelea kusisitiza
maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho ya kuitisha mikutano ya hadhara
nchi nzima kuanzia Septemba Mosi, ikiwa ni sehemu ya kampeni
itakayoendeshwa na Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), ambayo
tayari baadhi ya wakuu wa mikoa wamepiga marufuku.
Chadema
inadai kuwa uamuzi wa Rais kupiga marufuku mikutano ya kisiasa na
kudhibiti wanasiasa kuhudhuria mikutano hiyo nje ya maeneo yao, ni
kukiuka Katiba, Sheria ya Vyama vya Siasa, Kanuni za Maadili za Vyama
vya Siasa na haki za binadamu.
Kuhusu vita dhidi ya ufisadi, Rais pia aliahidi kuongeza kasi kupitia mtindo wake wa kutumbua majipu, huku akilishukuru Bunge kwa kupitisha sheria itakayosaidia vita hivyo pamoja na kupitisha bajeti ya Sh2 bilioni ya kuanzisha Mahakama Maalumu ya Rushwa.

Akizungumzia
suala la chakula nchini, Rais John Magufuli amewaagiza wakuu wa mikoa
na wilaya kuhakikisha maeneo yao yanazalisha chakula cha kutosha, akionya kuwa Serikali haitatoa chakula cha msaada kwa watakaokumbwa na njaa kutokana na uzembe na uvivu.
Rais
alisema kazi ya kulisha familia ni jukumu la wakuu wa familia na
kuongeza kuwa kila familia ina wajibu kulima na kuhifadhi chakula cha
kutosha mahitaji ya kipindi chote cha mwaka.
“Kazi
ya Serikali ni kutoa huduma kama barabara, dawa na mahitaji mengine ya
kijamii, lakini si msaada wa chakula kwa watu wavivu,” alisema Rais Magufuli.
Kuhusu
usafiri wa Reli ya Kati, Rais alisema tayari Serikali imetengeneza
zaidi ya Sh1 trilioni kwa ajili ya mradi wa kubadili reli hiyo kuwa
katika viwango vya kimataifa.
Alisema serikali pia inakusudia kununua meli mpya ya abiria itakayokuwa ikifanya safari Ziwa Victoria yenye uwezo wa kubeba abiria 1,000 na tani 800 ya mizigo.
Alisema serikali pia inakusudia kununua meli mpya ya abiria itakayokuwa ikifanya safari Ziwa Victoria yenye uwezo wa kubeba abiria 1,000 na tani 800 ya mizigo.
Pia
alisema Serikali imeweka mikakati ya kukabiliana na uvuvi haramu kwenye
Ziwa Victoria, ambalo lilikuwa likitoa fursa za ajira kwa watu zaidi ya
milioni 6 katika nyanja mbalimbali, fursa ambazo alisema zimepungua
maradufu kutokana vitendo vya uvuvi haramu.
Rais
Magufuli, ambaye atatumia ziara yake kukagua miradi ya maendeleo
ikiwamo ujenzi wa daraja la juu la waenda kwa miguu eneo la Furahisha
pamoja na upanuzi wa barabara ya Ghana-Pasiansi kutoka njia mbili za
sasa hadi nne, leo anatahutubia mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya
Furahisha, Kirumba jijini Mwanza.