Jokate
Mwegelo amesisitiza kauli yake aliyoitoa kwenye Instagram mwezi
uliopita kuwa anatamani kuona Alikiba na Diamond siku moja wanafanya
collabo.
Akiongea
kwenye kipindi cha 5 Select cha EATV hivi karibuni, Jokate alidai kuwa
ili collabo hiyo iwe nzuri, ni muhimu iwe halisi na wala isilazimishwe.
“It’s
has to be natural for it to be great,” alisema Jokate na kudai kuwa ni
Diamond na Alikiba ndio kiini cha muziki wa Bongo Flava kwa sasa.
Pia
alidai kuwa haoni sababu tena ya kujenga bifu na ex wake, Diamond
kwakuwa ameshakua kiumri na kwamba ni muhimu kushirikiana ili kuonesha
ushawishi wao.
Hata hivyo Jokate aliendelea kusisitiza kuwa yeye na Alikiba ni marafiki tu na kukanusha kuwa na uhusiano.
“We are just friends, we are better than that,” alisema.