Mkali ‘Kidogo’, Diamond Platnumz amepanga albamu yake atakayoiachia kabla ya mwaka kumalizika kuiuza hadi nje ya Tanzania.
Muimbaji
huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa yeye ni
msanii wa kimataifa na kwamba anafuata nyayo za kina Usher.
“Ukisema
utatoa album halafu unauza ndani tu ndio nini sasa, tunataka ukitoa
album iuzwe kama zinavyouzwa album za kina Usher huko, sasa hivi na mimi
nipo kimataifa,” alisema Diamond.
Ni
muda mrefu Diamond amekuwa akiahidi kuachia albamu yake mapema, hata
mwezi Februari mwaka huu kupitia akaunti yake ya Instagram aliandika,
“Albamu yangu mpya, ngoma mpya na albam ya Harmonize, na ujio mpya wa
Raymondtiptop. Soon zitakuwa masikioni mwako.”