Utangazaji nia ya kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) umeanza kwa kishindo, huku machifu wote wa Mkoa wa Mbeya wakitarajiwa kumuunga mkono Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya, ambaye leo anatarajiwa kutangaza nia mkoani Mbeya.
Miongoni mwao ni Chifu wa Rungwe, Mbozi na Chifu wa Jiji la Mbeya, Mwashiga ambaye atawaongoza pia wazee wote wa jiji hilo.
Wakati
hayo yakijiri, wakazi wa Jiji la Mbeya wakiwamo vijana, pia
wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kumsindikiza Profesa Mwandosya
kutangaza nia.
Hafla
hiyo inayotarajiwa kufanyika saa nne asubuhi, itafanyika katika ukumbi
wa mikutano wa Mkapa uliopo eneo la Soko Matola jijini Mbeya.
Katika
hafla hiyo, viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa vilivyo nje ya Ukawa
wanatarajiwa kuhudhuria ikiwa ni pamoja na kupata nafasi ya kutoa
msimamo wao wa kumuunga mkono Profesa Mwandosya.
Vyama hivyo ni TLP, ACT-Wazalendo, APPT- Maendeleo, UDP, PP, SAU na UPDP.
Wakati
Mwandosya akiwa Mbeya, Mbunge wa Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere
naye anatarajia kutangaza nia ya kuwania urais kijijini kwao Mwitongo
wilayani Butiama.
Ngeleja na Titus Kamani Kesho
Wakati
hayo yakijiri, Mbunge wa Sengerema mkoani Mwanza, William Ngeleja
pamoja na Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Titus Kamani wao
wakitarajiwa kutangaza kesho jijini Mwanza.
Nyalandu na Fomu
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema siku saba zijazo
kuanzia sasa atachukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kugombea urais wa Tanzania.
Alitoa
kauli hiyo jana jijini Arusha baada ya kumalizika ibada ya kwanza
aliyoshiriki katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),
Dayosisi ya Kaskazini Kati, Usharika wa Arusha mjini.
“Nimekuja
kanisani kuabudu, nimefarijika kwa neno la Mungu. Nataka kusema,
nilishatangaza nia miezi saba iliyopita, Desemba mwaka jana,” alisema
Waziri Nyalandu na kuongeza:
“Nia
haitangazwi mara mbili na siku saba baada ya miezi saba kuanzia sasa
hivi nitachukua fomu, historia itaandikwa upya ya nchi yetu, amani iwe
nanyi,” alisema Waziri Nyalandu.
Membe Juni 6
Kwa
upande waje Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard
Membe, amesema atatangaza nia ya kuwania urais Juni 6, mwaka huu
jimboni kwake Mtama mkoani Lindi.
Kutokana
na utangazaji nia unaoendelea sasa, amewataka Watanzania kuwapima na
kuwachunguza viongozi wanaojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi
katika Uchaguzi Mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba.
Akizungumza
jana wakati wa tamasha la kaswida lililoandaliwa na Taasisi ya Ulamaa
Promotion Centre, Membe alisema ni muda mwafaka sasa wa kuwapima
wagombea na matendo yao.
0 comments:
Chapisha Maoni