Serikali
imesema imefungua jalada la uchunguzi kuhusu mwanamke aliyejifungua
sakafuni katika kituo cha polisi Mang’ula wilayani Kilombero katika Mkoa
wa Morogoro, Amina Mapunda.
Kauli
hiyo imetolewa bungeni leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Yusuph Hamad Masauni alipotakiwa na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge
kutoa ufafanuzi wa Serikali kuhusiana na suala hilo.
“Tukio
lililotokea huko Morogoro ni la ovyo kabisa na la kinyama na Serikali
mnaweza kutoa kauli hapa na taifa likasikia,” amesema Chenge.
Akitoa kauli ya Serikali, Masauni amesema tayari jalada la uchunguzi limefunguliwa ili hatua kali za kisheria zichukuliwe.
“Tukio
hilo lilimhusisha mume wa huyu mama ambaye alinunua kitanda cha wizi na
polisi walipokwenda kwake wakakuta hicho kitanda cha wizi.
“Hivyo
wakamkuta mke wake wakamchukua kwa ajili ya mahojiano, kitu ambacho
hakikuwa sawa katika mazingira ya kawaida busara ingetumika.
“Hivyo serikali tumelichukulia kwa uzito suala hili na tunaendelea na uchunguzi halafu hatua kali zitachukuliwa,” amesema.
0 comments:
Chapisha Maoni