Zahanati
ya Kijiji cha Izinga, Kata ya Wampembe wilayani Nkasi mkoani Rukwa,
imefungwa kwa muda usiojulikana baada ya wakazi wa kijiji hicho kumkataa
mganga wa zahanati hiyo wakimtuhumu kuiba dawa.
Mwenyekiti
wa kijiji hicho, George Fataki alisema wananchi hao wamefikia uamuzi
huo baada ya kukamata dawa zikiuzwa katika duka la dawa za binadamu
kijijini hapo.
Alisema baada ya wananchi hao kumhoji mmiliki wa duka hilo alieleza kuwa dawa hizo aliuziwa na mganga huyo (jina tunalihifadhi).
Fataki
alisema baada ya wananchi hao kupata taarifa hizo walimfuata mganga
huyo na walipomhoji alikiri kumuuzia dawa mfanyabiashara huyo baada ya
kuona zimekaa muda mrefu bila kutumika na muda wake wa kufikia mwisho wa
matumizi ukikaribia.
Alisema
Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Hashim Mvogogo
alifika kijijini hapo kwa ajili ya shughuli za kikazi na kukuta mgogoro
huo.
Kwa
mujibu wa Fataki, kaimu mganga huyo alizungumza na wananchi ili
wamuache mganga huyo aendelee kutoa huduma katika zahanati hiyo.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Misana Kwangula alikiri kuwapo kwa
tukio la kufungwa kwa zahanati hiyo na kuongeza kuwa tayari muuguzi huyo
alikwisha fikishwa katika mikono ya sheria.

0 comments:
Chapisha Maoni