test

Jumatatu, 14 Mei 2018

Breaking News: Lulu Michael Yupo Huru......Kabadilishiwa Adhabu na Kupewa Kifungo Cha Nje


Mcheza filamu, Elizabeth Michael maarufu Lulu amebadilishwa kifungo na sasa atatumikia adhabu hiyo akiwa nje yaani ‘kifungo cha nje’.

Lulu, alishtakiwa kwa kesi ya kumuua bila kukusudia, aliyekuwa muigizaji maarufu wa filamu nchini na nje ya nchi, Steven Kanumba ambaye pia alikuwa mpenzi wake.

 
Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje amesema Lulu amebadilishiwa adhabu  na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.

“Lulu amebadilishiwa adhabu na ameachiwa juzi Jumamosi kati ya saa 2 hadi 3 asubuhi. Hii si kwamba ameachiwa huru, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo chake nje, kitaalamu tunaita ‘community service’” amesema Mboje

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni