Mjengo anaoishi mkali wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma yake ya Chekecha Cheketua, Ali Saleh Kiba.
Musa Mateja
Mjengo anaoishi mkali wa
Bongo Fleva anayetamba na ngoma yake ya Chekecha Cheketua, Ali Saleh
Kiba uliopo Kunduchi-Mbezi Beach jijini Dar, unadaiwa kuzua utata mkubwa
hivyo kulilazimu Risasi Jumamosi kuchimba na kubaini kuwa nyumba hiyo
si ya msanii huyo bali amepangisha.
Mkali wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba.
Awali, Kiba alikaririwa
akisema kuwa, mjengo huo wa kifahari ni wa ndugu yake aliyepo nje ya
nchi ambaye alimpa ili aishi na ndugu zake (wa Kiba) wakati yeye
(mmiliki) akiwa hayupo.Siku kadhaa mbele, baada ya Kiba kuvamiwa
nyumbani hapo na watu kupora vitu huku akinusurika kuuawa, jamaa huyo
alikaririwa redioni na kwenye mitandao ya kijamii akisema kuwa nyumba
hiyo ni yake.
Ilidaiwa kwamba, mara tu
baada ya Kiba kutangaza kumiliki nyumba hiyo, ilidaiwa kuwa aliibuka
mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Mariana ikisemekana eti ndiye
mmiliki halali wa nyumba hiyo.Madai mazito yaliendelea kushushwa kwamba,
Mariana, akiwa mwandani wa Kiba ndiye aliyemuweka Kiba aishi kwenye
nyumba hiyo wakati yeye (Mariana) kwa sasa anaishi nchini Singapore
barani Asia.
“Ninyi mnasema ule
mjengo ni wa Ali (Kiba)? Acheni hizo, kwa taarifa yenu hiyo nyumba
kapewa na mrembo f’lani hivi amazing, anaitwa Mariana, ni Mbongo
anayeishi Singapore.
“Muulizeni huyo Kiba
awaambie ukweli,” kilisema chanzo chetu kikisisitiza: “Hata Mariana
aliposikia eti nyumba ni ya Ali (Kiba) alishangaa na akamaindi ile mbaya
hivyo kwa sasa sidhani kama wanaelewana kwa ajili hiyo.”
Baada ya kukutana na
mkanganyiko huo, gazeti hili lilimtafuta Kiba ambaye alikiri kwamba
kweli nyumba hiyo siyo yake bali amepangisha huku akikana kusema kuwa
anaimiliki.Alipoulizwa juu ya madai ya kupewa nyumba hiyo na mwanamke
aitwaye Mariana, Kiba alisema hayo ni maneno tu kwani anachojua yeye
amepangisha.
“Kwanza hebu nitumie picha nijue ni nyumba gani?” aliomba Kiba ambapo alitumiwa picha kwa WhatsApp ndipo akajibu:
“Okey, kama ni hiyo nimepangisha lakini siyo kwamba sina nyumba.”
0 comments:
Chapisha Maoni