Mahakama
ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, imemhukumu kifungo cha miaka 3 jela
Immani Andongwisye (20), mkazi wa Kijiji cha Katumba Kata ya Kibisi
wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwa kosa ya kujaribu kumbaka bibi wa miaka
70.
Bibi aliyenusurika kufanyiwa kitendo hicho ametajwa kwa jina la Rahab Salesi, 70 mkazi wa kijiji na kata hiyo.
Akisoma
shtaka hilo Jumatano, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama hiyo, Patrick
Maliyabibi, alidai kwamba mstakiwa huyo alitenda kosa hilo Aprili 18
mwaka huu saa 2:00 usiku alipoingia ndani ya nyumba ya mama huyo.
Alidai
mshtakiwa alipoingia ndani alimvua nguo bibi huyo kwa nguvu kisha
kuanza kumtomasa tomasa maeneo mbalimbali ya mwili wake, akitaka
kumwingilia kimwili, lakini bibi huyo alijiangusha chini kutoka kwenye
kitanda.
Maliyabibi
aliiambia mahakama kuwa baada ya kujiangusha chini, alichukua panga
chini ya uvungu wa kitanda kisha kumkata kidole kijana huyo, ambaye
alikimbia.
Baada
ya Andongwisye kukimbia, bibi huyo alikwenda kwenye uongozi wa kijiji
usiku huo kutoa taarifa ambapo alikamatwa na kupelekwa polisi mjini
Tukuyu.
Aliongeza
kuwa baada ya kuwekwa lumande alifunguliwa kesi namba 38 na kuanza
kusikilizwa katika mahakama hiyo huku mashahidi wa upande wa mashtaka
wakipeleka ushahidi.
Mwendesha
Mashtaka huyo aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa huyo,
ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaofanya vitendo hivyo kwa kuwa
suala hilo linawadhalilisha wanawake ambao wengi wao ni wajane.
Akitoa
hukumu hiyo, Hakimu Aristrida Tarimo, alisema ameridhika na ushahidi
iliotolewa na upande wa mashtaka, hivyo kumhukumu kutumikia kifungo cha
miaka 3 jela, ili iwe fundisho kwa wengine.
Nje
ya mahakama, baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Katumba, walisema
mahakama imetenda haki kwa kuwa kitendo kilichofanywa na kijana huyo ni
cha udhalilishaji.
0 comments:
Chapisha Maoni