Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Mhe. Mizengo Pinda amesema yeye hana kinyongo na uteuzi wa Dk. John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM.
“Tulikuwa
wengi kwenyhe kinyang’anyiro cha urais lakini Makamu wa Rais ametolewa,
Waziri Mkuu aliyepo ametolewa, Mawaziri Wakuu wastaafu wametolewa,
Majaji na mabalozi wametolewa, mawaziri wengine wametolewa; hivi ni kwa
nini useme kwamba wewe tu ndiye unayefaa kuteuliwa? Ni kwamba Mungu
alikwishamuandaa mmoja wetu,” alisema.
Ametoa
kauli hiyo jana wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wakazi wa
jimbo la Mpanda Vijijini kwenye mikutano minne ya hadhara iliyofanyika
katika kata za Kasekese, Kapalamsenga, Karema na Ikola.
“Magufuli
ni muadilifu, ni mchapakazi, hana blah blah za kisiasa na hapendi
rushwa. Ni mtu anayetaka kuona matokeo na mwenye kujali watu wanyonge.
Nimefanya naye kazi kwa muda mrefu, ninamfahamu, ninaomba mumpe kura ya
ndiyo ifikapo terehe 25 Oktoba,” alisema Mhe. Pinda wakati akimuombea kura Dk. Magufuli.
Akizungumzia
mafanikio ya serikali ya awamu ya nne, Mhe. Pinda alisema Serikali ya
CCM imefanya kazi nzuri kwa kufungua barabara za vijijini akitoa mfano
wa barabara ya Mpanda hadi Karema ambayo alisema imeboreshwa tofauti na
ilivyokuwa miaka 10 iliyopita.
“Wakati
huo ukitoka Mpanda kuja Karema ilimchukua mtu hadi siku tatu wakati ni
umbali wa km. 150 tu… leo hii mtu anatoka Karema hadi Mpanda na
kuunganisha mabasi ya Mwanza siku hiyo hiyo,” alisema.
Alisema
katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015, Serikali ya awamu ya tano
imepanga kujenga reli mpya ya viwango vya kimataifa (standard gauge)
kutoka Kaliua kupitia Mpanda hadi Karema. Alisema anaamini reli hiyo
itakuwa ni kiungo cha kuleta maendeleo ya haraka kwenye ukanda huo wa
Magharibi.
Alisema Seikali itaendelea kuwaletea maendeleo wanandhi ikiwemo kubotesha huduma za maji, umeme na mawasiliano ya simu.
Aliwataka
wakazi wa jimbo hilo watunze shahada za kupigia kura na wasikubali
kurubuniwa na mtu yeyote iwe kwa fedha au kitu chochote.
“Usikubali
kumpa mtu shahada yaka hata kama ni motto wako. Ninawasihi mjitokeze
kwa wingi siku ya kupiga kura wala msisikilize vitisho vya mtu yeyote
kwamba hakutakuwa na amani,” alisema.
Mhe.
Pinda alitumia fursa hiyo kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Mpanda
Vijijini, Bw. Selemani Moshy Kakoso pamoja na madiwani wa kata zote nne.
Akiwa Karema, Mhe. Pinda alipokea kadi za wanachama waliorejea CCM kutoka vyama vya CHADEMA NA ACT Wazalendo.
0 comments:
Chapisha Maoni